Kuzaliwa Imam Hasan Askariy

  • Habari NO : 260065

Imam Hassan Askary(A.S) sala na amani ziwe juu yake, ni Imam wa Kumi na moja wa Mashia na ni baba Mtukufu wa Imam Zamani(Roho zetu zipo kwa ajili yake). Yeye alizaliwa katika siku ya tarehe Nane Rabii Thani mwaka 232 Hijria, Qamary. Jina lake la kunia ni Abu Muhammad na laqabu yake ni Swaamit, Hadi, Siraj, Rafigh, Zakii, Naqii, na Askary. Katika umri wake mtukufu alikuwa chini ya himaya ya Banii Abbas, na alistahamili misukosuko na mateso mengi hadi pale mtukufu huyo alipobadilisha makazi na kwenda katika mji wa Samaraa, na akawa karibu na majeshi ya utawala wa Abbas.

Ukarimu na Utukufu wa Imam huyu ni zaidi ya kile kilicholetwa katika mukhtasari huu, na moja kati ya Makarama yake ni kwamba, kikundi cha watu kutoka uko wa Banii Abbas waliingia kwa Swaleh bin Wasif na wakataka ateswe kupitia kwake , kwani Imam Askary(A.S) alikuwa katika jela yake, ampe mateso. Swaleh aliwaambia hivi: Mimi yeye nimfanye nini? Hali ya kuwa mimi nilikuwa na watu wawili ambao niliwajuwa kwa uovu wao mkubwa na niliwatuma kwake, lakini kila mmoja wao alimbadilisha akawa mtu wa ibada na sala na funga, na katika jambo hili kazi yake ikafanikiwa!

Aliamrisha watu hao wawili watolewe na waletwe mbele yake, na akawaambia wale watu wawili: Ole wenu! Juu ya mtu huyu muliona hali gani kwake? Wale wafungwa wawili walimwambia Swaleh: Tuseme nini kuhusu mtu ambaye mchana wote hufunga, na usiku wote hukesha kwa ibada, hazungumzi, na hafanyi kazi yoyote isipokuwa ibada. Pindi anapotuangalia sisi kuwa tunatetemeka na hututokea hali Fulani ambaye huwa hatujitambui! Bani Abbas baada ya kusikia habari hizi walivunjika moyo na wakarudi hali ya kuwa ni wenye kukata tamaa.

Mtukufu huyo baada ya kupita umri wake mtakatifu wa miaka 28, katika mwaka wa 260 Hijria, Qamary alifikisha Shahada yake kwa athari ya sumu, ambayo alipewa na Khalifa wa wakati huo, na jukumu la uyatima likaangukia juu ya uso wa Imam Zamani(A.S).

Kaburi lake tukufu liko katika mji wa Samara na kwa miaka mingi imekuwa ni sehemu ya ziyara ya marafiki wa Ahlul Bait. Kwa sasa ni miaka mingi imeshapita tangu kuharibiwa na kuvunjwa na waovu na maadui wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake(S.A.W.W) , na tunatarajia ya kwamba litajengwa kwa haraka sana, na kwa ubora na uzuri zaidi kuliko lilivyokuwa mwanzoni.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni