Historia ya Waja wema

Muhtasari wa maisha ya Fatimah Zahra

  • Habari NO : 268141
  • Rejea : ABNA

Yeye ni Fatima Zahraa (a.s) baba yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) Mohammad bin Abdillah na mama yake ni Sayyidah Mtukufu Khadijah (a.s) mama wa waumini na mumewe ni bwana na wasii wa Mtume Ali Amirul muuminiin na watoto wake pia wajukuu wake ni maimam watwaharifu (a.s).

Alizaliwa (a.s) tarehe (20) ya mwezi wa Jamaddul-akhir mwaka wa (45) tangu kuzaliwa Mtume (s.a.w) na alikufa shahidi akiwa ni mwenye kudhulumiwa tarehe 3 Jamaadul Aakhir siku ya juma nne mwaka wa kumi (11) hijiria akiwa na umri wa miaka (18) katika umri wa kuchanua maua waridi (yaani katika umri wa ujana wake).

Na Amirul muuminiin ndie alie simamia suala la kuandaa mazishi yake na kumzika katika mji wa madina na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake ikiwa ni hoja kutokana na dhuluma aliyo fanyiwa na haki yake iliyo porwa na kuchukuliwa kwa nguvu.

Na Fatima alikuwa kama baba yake katika ibada na uchamungu na ubora na Zuhdi, na Mwenyezi Mungu aliteremsha aya kadhaa kuhusiana na hadhi yake (kuhusiana nae).

Na Mtume (s.a.w) ndie alie muita kwa laqabu (jina mashuhuri) ya (Sayyidatu nisaail aalamiin) Mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na kumuita kwa kunia ya Ummu abiiha (Mama wa baba yake) na alikuwa akimpenda sana na kumtukuza sana na kwa kiwango kikubwa, hata ilifikia hatua kwamba anapo ingia kwa Mtume humkaribisha na kusimama kwa heshima yake na kumkalisha mahala pake na pengine alikuwa akiibusu mikono yake na Mtume (s.a.w) alikuwa akisema: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwa maridhio ya Fatima na anachukia kwa kuchukia Fatima.

Alimzalia Amirul muuminiin (a.s) watoto wafuatao: Imam Hassan (a.s) na Imam Hussen (a.s) na Muhsin (a.s) lakini Muhsin mimba yake ilitoka kabla ya muda wake kutokana na maudhi na masaibu yaliyo mfika mama yake, na Sayyidatu Zainab (a.s) na Sayyidah Ummu kuluthuum (a.s).


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni