Historia ya waja wema

Imam Sadjad(a.s)

  • Habari NO : 268990
  • Rejea : Ripoti ya ABNA

Yeye ni Imam Ali bin Hussen (a.s) na mama yake ni Shahri banuu binti wa mfalme Yazdjard na Imam huyu (a.s) alikuwa akiitwa Mtoto wa wateule wawili, kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w): Hakika mwenyezi Mungu ana wateule wawili katika waja wake, mteule wake katika waarabu ni Quraishi na katika waajemi (wasio waarabu) ni ni Mfursi na kwa kuyazingatia maana ya maneno haya Abul Aswad akaimba shairi lifuatalo: Hakika mtoto alie zaliwa kati ya Kisraa na Haashim ni mkarimu zaidi ya watoto wote walio vishwa hirizi shingoni mwao.

Amezaliwa (a.s) katika mji wa Madinanatul-munawwarah siku ya Ali-khamisi mwezi mtukufu wa Shaaban [19] mwaka (38) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma mosi tarehe (25) mwezi wa Muharram  mwaka (95) akiwa na umri wa miaka (57), na mwanae Imam Baaqir (a.s) ndie alie simamia suala la mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la Ami yake Imam Mujtaba (a.s) katika mji wa madinatul-munawwarah.

Na alikuwa ni wa aina yake (kwa maana ya kuwa hakuwa na mfano) katika zama zake katika suala la elimu, ibada, fadhila, uchamungu, kuwasaidia watu wenye kuomba misaada na wenye kutaka usaidizi na mengineyo, na maulamaa wengi pia mafaqihi wamepokea riwaya nyingi sana na zisizo hesabika kutoka kwake na kuhifadhi kutoka kwake dua na mawaidha mengi na karama mbalimbali na mengine mengi yasiyo hesabika.

Na alikuwa akitoka usiku wa kiza na kubeba mfuko mabegani mwake ukiwa na Dinari na Dirham napengine alikuwa akibeba mgongoni mwake mfuko wa vyakula, au kuni na kupita mlango mmoja mmoja akibisha hodi na kumpatia kila atokae kwenye nyumba hizo pesa hizo, na alikuwa akifunika kichwa chake ili mafakiri wasimfahamu, na pindi alipo fariki watu wa madina wakafahamu na kuelewa ya kuwa yeye (a.s) ndie ambae alikuwa akibeba mfuko na kuwapatia vyakula.

Pamoja na hayo akipendezewa sana kula pamoja na mafukara au kuhudhuria kwenye chaku chake mayatima na mafakiri na kula pamoja nae.

Na miongoni mwa tabia zake njema (a.s) ni kuwa katika kila mwezi alikuwa akiwaita wahudumu wake na kusema: Mwenye kutaka kuolewa kati yanu nitamuoza, au akitaka kuuzwa nitamuuza, au akitaka kuachiwa huru nitamuachia huru.

Na pindi alipokuwa akijiwa na muombaji husema: Karibu wewe ambae huibeba akiba yangu ya akhera.

Na kutokana na uchaji mwingi wa mola ni kuwa alikuwa akisali kwa usiku na mcana wake rakaa elfu mmoja na anapo kuwa kwenye sala ngozi yake husinyaa na kukunjamana na rangi yake kubadilika na kuwa ya njano na kutetemeka kama kuti la mtende, na miongoni mwa laqabu zake ni Dhuthafanaati (mwenye sugu au magamba), kutokana na athari za sajda katika paji lake la uso na vitanga vyake pia magotini mwake.

Mtu mmoja alimtusi na kumtolea maneno machafu na mabaya na yeye (a.s) akiwa kimia hazungumzi wala kasema chochote na baada ya muda Imam (a.s) akamwendea, waliokuwa wamehudhuria wakadhania ya kuwa anataka kumfanya kama alivyo fanya yeye, mara akasoma aya ifuatayo:

(والكاظمين الغيظ والعافين عن الناس والله يحب المحسنين)

Na wenye kuvunja ghadhabu na kuwasamehe watu na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema.

Kisha akamsimamia bwana yule na kusema: Ewe ndugu yangu hakika wewe ulisimama kwangu (ulinisimamia) muda ulio pita na kusema uliyo yasema, ikiwa umeyasema kwangu hayo uliyo yasema, basi mimi nina muomba Mwenyezi Mungu msamaha na ikiwa umesema mambo ambayo siko nayo, Mwenyezi Mungu akusamehe.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni