Imam Husein(as)

Udongo wa Karbala kugeuka damu siku ya Ashura+ Picha

  • Habari NO : 368176
  • Rejea : abna
Siku ya Ashura udongo wa kaburi la Imam Husein(as) kugeuka damu katika makumbusho ya Karbala.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul bayt(as)-ABNA- Tukio la huzuni lililotokea miaka 1400 ilopita katika Mkoa wa Karbala kuuawa mjukuu wa Mtume Muhammad(saw) Imam Husein Ibn Abi Talib(as) lilitikisa mbingu na ardhi kwa kuuawa kipenzi cha Mtume(saw).

Tukio la kugeuka damu udongo huu wa kaburi la Imam Husein(as) lilitokea machoni mwa watu walokuwa katika makumbusho hayo.

Aidha tukio hili ni hikaya kutoka kwa Mtukufu Mtume(saw) alipomshukia Jibril(as) akija na udongo wa Karbala akimletea Mtume(saw) habari za shahada na kifo cha Imam Husein(as), Na Mtume(saw) udongo huo alimkabidhi Ummi Salamah na kumueleza kua: Udongo huu utakapogeuka rangi nyekundu basi fahamu kua mwanagu Husein kaishauawa katika ardhi ya Karbala.

Kisa hiki kimenakiliwa pia katika Vitabu vya Sunni na Shia kama; Ibn Hajar Al-Askalani katika Kitabu chake Tahdhibu Al-Tahdhib, Ibn Abi Bakr Haithami katika Kitabu chake Majmaa Al-Zawaid na Tabrani katika Kitabu chake Al-Muujamu Al-Kabir.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni