Kuzaliwa Bibi Fatima Maasuma(as)

  • Habari NO : 460301
  • Rejea : ABNA.co
Brief

Alizaliwa katika mji wa Madina watu wakiwa na shauku ya kumuona mtoto atakayezaliwa kutoka katika familia ya Mtume wetu mtukufu (s.a.w) na katika nyumba ya Imamu Kaadhimu (a.s) iliyokuwa imezongwa na furaha kwa kukaribia kuzaliwa kipenzi cha nyoyo zao.

Mke wa Imamu Kadhimu (a.s) aliyekuwa akiitwa Najma alizidi kuwa na furaha siku baada ya siku kutokana na shauku ya kuzaliwa mtoto.

Hatimaye mwanzoni mwa dhulkaada (mwezi wa kumi na moja) katika mwaka wa 173 “H” ilitimia ile siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa baina ya watu wa familia hiyo. Ni siku hiyo ambayo aliruzukiwa Imamu Kaadhimu (a.s) kutoka kwa mola wake mtoto wa kike msifika na aliyehifadhika, na ilikuwa ni siku ambayo furaha iliizonga sana jamii na hasa familia ya Imamu Kaadhimu kutokana na rehema hiyo waliyoletewa. mkewe Imamu alikuwa na furaha ambayo haiwezi kumithilika kutoka kwa Mola mwingi wa rehema kwa kuwaruzuku mtoto wa pili aliyejaaliwa kila aina ya rehema baada ya yule wa kwanza aliyezaliwa miaka ishirini na mitano iliyopita.

Aliyeitwa Ally ambaye pia alijulikana kama Ridhaa. Yeye pia alikuwa amezaliwa katika mwezi kama huo dhulkaada katika mwaka wa 148 “H”. Na pia hiyo ilikuwa ni furaha ya pili kwa

Imam Kaadhim baada ya ile ya kwanza ya kuzaliwa Imamu Ridhaa (a.s).

Baada ya kuzaliwa Imam Ridhaa ilipita tena miaka mingi kabla ya bibi Najma mkewe Imam (a.s) kujaaliwa mtoto mwingine na hivi sasa amejaaliwa mtoto mwingine wa kike ambaye atakuwa ni dada yake Imamu Ridhaa (a.s)

Kutokana na mapenzi mazito aliyokuwa nayo Imamu Kaadhim (a.s) juu ya bibi yake mpenzi na mtoto wa Mtume Mtukufu (s.a.w) na mke wa Imamu Ally (a.s) Faatwima Zahraa, aliamua kumuita mtoto wake huyo aliyezaliwa kwa jina la bibi yake huyo Fatima (a.s) ambapo kutokana na uchamungu wake na ibada zake alijulikana kama Maasumah.

Jina la Fatuma kwa Ahlulbayt (a.s) lina mahali makhsusi kwenye nyoyo zao, kwani linawakumbusha matamu na machungu aliyoyapitia bibi Fatima Zahraa (a.s). Na wanapompa mmoja katika mabinti zao jina la Fatima, huwa wanamtaza na kumpa heshima makhsusi kwa kuwa jina lake limefanana na jina la kipenzi cha mtume (s.a.w.) hivyo basi sunna hii nzuri ilimhusu bibi Fatima Maasuma (a.s) pia.

Imam naye Kadhim (a.s) alijitahidi awezavyo katika kuchunga malezi ya binti yake huyu na kudhihirisha mapenzi yake kwake.

Sayyida maasuma aliishi chini ya malezi mema ya wazazi wake watukufu. hivyo basi kutokana nao aliweza kupata utukufu na hashima. Kwa kuwa baba yake alikuwa ni Imam Maasum ambaye hakuna aliyemfikia (katika zama zake) kwa utukufu na ucha Mungu. Na mamae alikuwa ni miongoni mwa mabibi wema na waumini ambaye alijifunza katika chuo cha mke wa Imam Swadiq (a.s) ambaye pia alijulilkana kwa uchamungu katika zama hizo. Na hapa ndipo tunamkuta bibi (Hamida) mamae Imam Kaadhimu (a.s) akimuelekeza Imam Kaadhimu (a.s) kumuoa bibi Najmah.

Sayyida Maasumah (a.s) kila siku alikuwa akifaidika kutokana na babae na ndufuye waliekuwa ni Maasum (a.s) na mamaye pia ambaye alikuwa mcha mungu mwenye elimu na kuweza kufikia cheo cha juu cha elimu na utukufu na hivyo basi

Kuwa mjuzi katika mambo mbalimbali ya dini hii tukufu angali akiwa na umri mdogo.

 Ilitokea siku moja lilikuja kundi la shia katika mji mtuukufu wa Madina ili waweze kuelezwa na kujibiwa baadhi ya masuali ya dini waliyokuja nayo kwa Imamu Kaadhim (a.s) ili waweze kupata elimu kutoka kwake kwa kujibiwa maswali yao. lakini kwa bahati mabaya Imamu alikuwa ametoka pamoja na mtoto wake mpenzi Imam Ridhaa (a.s) walikuwa wamesafiri nje ya mji wa Madina. lile kundi la watu lilihuzunika kwa kuwa  halikumkuta yule kipenzi chao na mja wa Mwenyezi Mungu yaani Imamu Kaadhim (a.s) mabaye walidhamiria kupata elimu kutoka kwake. Wala mwingine ambaye angeweza kuyajibu maswali yao hivyo baada ya majadiliano ya muda waliamua kurejea walikotoka hali ya kuwa wamejawa na majonzi na simanzi.

Fatuma Maasuma (a.s) alipowaona wale watu wakiwa katika hali ile ya majonzi aliyachukua maswali yao ambayo yalikuwa yameeandikwa na kisha akayajibu yote, na yalikuwa ni majibu ambayo hata wale wageni hawakutegemea, jambo hili lilipelekea wageni wale kubadili huzuni zao kuwa ni furaha kubwa na wakarejea hali ya kuwa ni wenye kufanikiwa katika jambo lile lililo waleta.

Lakini punde tuu walipotoka katika mji wa Madina wakiwa njiani kuelekea katika mji wao walikutana na Imamu Kaadhim (a.s) na wakamweleza yaliyowasibu, Imamu alipoona majawabu ya mwanaye kwa wageni hao, alishukuru kwa aliyofanya binti yake, na kwa ajili ya kumsifia binti yake kwa ibara ya maneno machache kwa kusema “Amemfidia babake”.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni