Mafunzo ya Jamii

Maana ya hadithi Thaqalaini- Sehemu ya kwanza

  • Habari NO : 474082
Brief

Tunajifunza kutokana na hadithi hii tukufu mambo yafwatayo:-

1– Mtume(s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kifo chake.

Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kuhusu kifo chake. Hadithi nyingi zinaonyesha maana hii, kama vile kauli yake tukufu aliyoisema;

((اني اوشك ان ادعى فاجيب))

“Hakika mimi huenda nikaitwa (na Mola wangu) nami nikajibu.”

Na kauli yake:

((ان الله عزوجل اوحى اني مقبوض))

“Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ameniteremshia wahyi (kunijulisha) kuwa mimi nitafariki”. Pamoja na kauli nyingi nyinginezo.

Hizi hadithi zinaonyesha kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alipozungumza maneno hayo alikua katika hali ya kubainisha wadhifa wa umma baada ya kufa kwake, ili usibaki katika hali ya kupuuzwa, jambo lisilomstahiki Mtume(s.a.w.a) kwani mfano wake, ambaye ni mwanzilishi wa uislamu, atawezaje kuridhia kuuacha uislamu na waislanu hivi tu, bila ya mwelekeo, baada ya kupitio mateso na misiba katika kuuasisi uislamu na serikali ya kiislamu? Kamwe, hekima ya Mwenyezi Mungu pamoja na elimu ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) haimruhusu yeye (s.a.w.a) kufanya vivyo.

2) Kutotengana kwa Qurani na kizazi cha Mtume (s.a.w.a)

Kuviacha vitu viwili (yaani Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ) katika umma ni sawa na kuvifanya kuwa makhalifa wake. Basi Quran na kizazi chake Mtume (s.a.w.a) ni makhalifa wawili wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) katika ummu. Vinachukua cheo cha Mtume (s.a.w.a) vinapo-dumu kuwa pamoja na kutofarikiana, na hii ndio sababu tunaona kwenye hadithi nyingi Mtume (s.a.w.a) akiviita makhalifa, kama alivyopokea Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kutoka kwa Zaid ibnu Thabit, aliyesema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema:

((اني تارك فيكم خليفتين))

“Hakika mimi ninaacha kati yenu makhalifa wawili”.([1])

Vile vile imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Alkhidri ya kwamba alisema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a.) alihotubia na kusema:

((يا ايها الناس اني تركت فيكم الثقلين خليفتين))

“Enyi watu, hakika mimi nimeacha kati yenu vizito viwili, vikiwa (kama) makhalifa wawili”. ([2])

Au kwa riwaya nyingine;

((اني مخلّف فيكم الثقلين))

“Hakika mimi ninaviacha viwili vizito kuwa makh-alifa kati yenu”.([3])

Na kwenye riwaya nyingine alisema:

((قد خلفت فيكم الثقلين))

“kwa hakika nimeviacha viwili vizito kuwa makhalifa kati yenu”.([4])

Lengo la kukifanye kizazi chake (s.a.w.a) kuwa khalifa na kukiachia cheo chake si jengine ila tu, ni kukipa majukumu yake, na hii kwa njia nyingine inathibitisha uimamu na uongozi wa kizazi chake (s.a.w.a) juu ya umma wake.

Kwa hivyo basi, hadithi hii inatuthibitishia vilevile uongozi wao katika mambo ya kisiasa kama inavyo-thibitisha uongozi wao katika mambo ya kielimu na mengineo. Inatuthibitishia pia wajibu wa kuwafuata kiujumla, na wala haikushurutisha jambo lotote lile katika kuwafuata. Imetuthibitishia pia uharamu wa kuwatangulia au kubaki nyuma (yao).

Lakini, ni sikitiko kubwa kuona kuwa umma wa kiislamu uliwaacha na kuwapuuza Ahlulbait (Baada ya kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ametilia mkazo sana.) na wala hawakujali haki zao, kwani hawaku-unyenyekea uimamu na uongozi wao, bali walifanya yale waliyoya fanya baada ya kuwa Mtume (s.a.w.a) amemteuwa na kumuainisha Imamu katika sehemu nyingi na hasa katika siku yake ya kuaga dunia.

Zaidi ya hayo hawakuchukuo hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu na wala adabu na sunna za Mtume (s.a.w.a) walibaki bila kuziandika hadi baada ya nusu ya karne ya pili ya hijriya takriban, ali po kuja khalifa Umar ibnu Abdul Aziz na kuifuta sheria hii, kwa kuona kuwa hadithi tukufu zina potea. Ndipo maula-maa wa kisunni wakaanza kuandika hadithi za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ziilizobaki (kama vile Malik na Ahmad ibnu Hambal na Bukhari na wengineo (kwa utaratibu huo) baada ya kuzisahao nyingi kati ya hizo au baada ya kufariki kwa kwa waliokuwa wamezihi-fadhi. Baadhi ya wachunguzi wa hadithi wamesema ya kwamba “Hadithi wanazozitegemea (ndugu zetu masunni) katika kutoa hukumu za sheria hazizidi mia tano”.

Na kwa hivyo sunna (hadithi) za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) kwa ndugu zetu masunni zilikuwa hazijaku-sanywa wala hawakuzijua kabla ya nusu ya karne ya pili, na hali ya kuwa sunna kamili ilikuwa pamoja na Ahlul bait (a.s) tangu kuaga dunia kwa Mtume (s.a.w.a).

Kwa hivyo basi, nini sababu ya kuiacha na kuipuuza elimu ya Ahlulbait, ilhali walikuwa wakina-kili sunna ya Mtume (s.a.w.a) kama ilivyo kuwa, kwa ukamilifu.

Almuhaqqiqul wahiid (Muhakiki wa aina yake) Seyyid Burujurdi (r.a) amesema ya kwamba, “Kuna hadithi nyingi zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul bait (a.s) zisemazo kuwa wana kitabu kilichoandikwa kwa imla([5]) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na kwa khati za Imam Ali bin Abi Talib (a.s), ambacho ndani yake kuna Sunna zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuyafikisha kwa umma wake, katika mafunzo na hukumu za kidini.”

Kisha alitaja baadhi ya riwaya hizi zenye kuon-yesha kuwepo kwa kitabu kwa imla ya Mtume (s.a.w.a) na kwa hati ya Ali (a.s) na kusema, “Inadhihiri kutokana na hadithi hizi mambo yafwatayo”.

Kwanza: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) hakuuacha umma baada yake bure, bila ya Imamu wa kuwaongoza, wala bayana ya kutosha, bali aliwacha-gulia Maimamu, watukufu, waongozao na kuihifadhi dini, kisha akawapa mafunzo yanayomhusu Mwenyezi Mungu, faradhi za kidini, sunna na adabu, halali na haramu, hekima na athari, na yote wanayoyahitajia watu hadi siku ya kiama, hata ikiwa mtu atamkwaruza mwenzake amewaelezea ni kiwango gani cha faini (dia) kinachofaa kutolewa. Wala hakumruhusu yeyote kuhukumu au katoa fatwa kwa kutumia rai na maoni yake au kwa kutumia Qiyas (kufananisha hukumu za sheria kama wafanyavyo ndugu zetu masunni) kwani hakuna maudhiu au jambo lolote lisilokuwa na hukumu thabiti itokayo kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mjuzi Mwenye Hekima, bali Mtume (s.a.w.a) alimju-lisha Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) sheria na hukumu zote na kumuamuru kuwa aziandike na kuzihifadhi. Na kuwakabidhi Maimamu (a.s) katika kizazi chake. Basi Ali (a.s) aliandika kwa hati yake (tukufu) na kuwakabidhi waliokusudiwa (yaani Maimamu).

Pili: Mtume (s.a.w.a) alimwamuru Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) peke yake kuandika na wala hakuna yeyote mwengine katika zama zake aliyejua aliyoku-wa ameandika. Kisha alimwusia kuwa kitabu hiki kiwe mikononi mwa Maimamu kumi na wawili baada yake. Basi inauwajibikia umma wote wa kiislamu kuchukua elimu inayo husu halali na haramu, na yote wanayohitajia katika dini yao kutoka kwake Ali (a.s) na Maimamu watokanao na kizazi chake, kwani wao ndio wasiri wa Mtume (s.a.w.a) na ndio hazina ya elimu yake na wahifadhio dini yake.

Tatu: Kitabu hiki kilikuwa mikononi mwao Maimamu (a.s). Imam Muhammad Baqir (a.s) na Imam Ja’afar Swadiq (a.s) waliwaonyesha baadhi ya maswahaba wao na wengineo katika wafuasi wa dhehebu la kisunni, ili kuitimiza hoja, na ili kuwaon-dolea shaka mioyoni mwao”.

REJEA TUTATOA MWISHO WA MLOLONGO WA MAKALA HIZI INSIHAALLAH


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni