MALEZI BORA KWA WATOTO

  • Habari NO : 694984
  • Rejea : ABNA
Brief

Hakika suala la malezi bora ni suala muhimu katika maisha ya mtoto kwa maana malezi bora ndio kipengere muhimu kinacholeta tofauti baina ya mwanadamu na viumbe vingine hai, hivyo kwa malezi bora ndio twaweza kumpata mwanadamu mwema vilevile kinyume chake

بسم الله الرحمن الرحیم
MALEZI BORA KWA WATOTO
Umuhimu wa malezi bora kwa mwanadamu
Namshukuru mola muumba kwa kunipa uwezo wa kuandika makala hii bila yakusahau shukurani sala na salamu kwa bwana wa walimwengu na manabii wote mtukufu mtume Muhammad na ahali zake watakatifu bila ya kuwasahau masahaba wema waliomfuata mtume kwa haki mpaka mwisho wa maisha yao.
Hakika suala la malezi bora ni suala muhimu katika maisha ya mtoto kwa maana malezi bora ndio kipengere muhimu kinacholeta tofauti baina ya mwanadamu na viumbe vingine hai, hivyo kwa malezi bora ndio twaweza kumpata mwanadamu mwema vilevile kinyume chake, kama alivyosema mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufuوَلَقَدْ ذَرَأْنا لِجَهَنَّمَ كَثِيراً مِنَ الْجِنِّ وَ الْإِنْسِ لَهُمْ قُلُوبٌ لا يَفْقَهُونَ بِها وَ لَهُمْ أَعْيُنٌ لا يُبْصِرُونَ بِها وَ لَهُمْ آذانٌ لا يَسْمَعُونَ بِها أُولئِكَ كَالْأَنْعامِ بَلْ‏ هُمْ‏ أَضَلُ‏ أُولئِكَ هُمُ الْغافِلُونَ Kwa hakika tumeuumbia moto wa Jahanamu wengi katika ya watu na majini, kwakuwa wana nyoyo lakini hawazingatii kwa nyoyo zao na wana macho lakini hawaoni kwayo na wana masikio lakini hawasikii kwayo basi hao ni kama wanyama bali wao wamepotea zaidi na hao ndio walioghafilika.
Moyo, macho na masikio nikatika vyanzo vya msingi vya mafunzo kwa mwanadamu ambavyo mwanadamu anatakiwa kuvitumia vyanzo hivi kwa mafunzo mema ambayo yatamfikisha katika ukamilifu na heshima yake ya kibinadamu, mwenyezi Mungu anasema katika Qur`an
  وَ اللَّهُ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُطُونِ أُمَّهاتِكُمْ لا تَعْلَمُونَ‏ شَيْئاً وَ جَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَ الْأَبْصارَ وَ الْأَفْئِدَةَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَدNa mwenyezi amewatoa katika matumbo ya mama zenu mkiwa hamfahamu chochote na akawapa masikio na macho na nyoyo ili muweze kumshukuru (surat Nahl 78).
Tukijumuisha aya hii na iliopita tunafaidika kuwa mwenyezi Mungu aliyetakasika aliviweka vyanzo hivi kwa lengo la kumpatia mwanadamu mafunzo mema yatakayoweza kukamilisha utu wake, huku akitaadharisha matumizi mabaya ya vyanzo hivi bila shaka si tu hatafikia lengo bali utukufu wa mwanadamu huyo utabadilika nakuwa dhalili kuliko vingine kama vile wanyama na kadhalika, na hapo ndipo hupatikana mwanadamu fasiki, dhalimu asiyejali haki za watu. Ubinadamu na utu kwakuwa hakuvitumia kupata malezi bora ya kibinadamu
Hatua za malezi bora
Kuhusu hatua za malezi bora kuna nadharia nyingi baina ya wataalamu wa elimu ya malezi ambao huzigawa hatua hizo katika vigawanyo vifuatavyo: 1- inapotunga mimba mpaka kuzaliwa 2- kutoka kuzaliwa mpaka miaka saba 3- kutoka miaka saba ya awali mpaka miaka saba ya pili 4- miaka saba baada ya miaka saba ya pili 5- hatua ya ukubwani. kwa ufupi tunaweza kusema ni hatua ya ufalme kwa mtoto, hatua ya utumwa katika maisha ya mtoto, hatua ya uwaziri na unaibu na  hatua ya utuuzima, pamoja kuwa Uislamu una hatua nyingine muhimu kinyume na hizi, nayo ni kabla ya kufunga ndoa na mama kushika ujauzito kwa maana malezi na mustakabali wa watoto unatabirika kutokana na familia na sifa za wanandoa wawili nami katika makala hii nitazungumzia suala hili kwa ufupi. Katika kufafanua hatua hii mtukufu mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema:{تزوّجوا في الحجر الصالح، فإن العرق دساس} oweni katika familia yenye maadili mema, kwa hakika asili ni yenye kujificha.
Hii ni kanuni ya maumbile ya kibinadamu kuwa watoto hufanana na wazazi wao na ndugu zao wakalibu kitabia mwenendo na maumbile, hivyo kama mmoja kati ya wazazi au ndugu zao watakuwa na sirika asi au anatoka katika familia inayosifika na tabia mbaya bila shaka kuna uwezekano mkubwa wa kuhamia silika hiyo kwa mtoto anayetarajiwa kupatikana kupata malezi bora baadaye, hivyo mtazamo wa Uislamu unalenga kutuzindua kuwa kila mtu anamiliki seli na chembechembe katika uwepo wake ambazo zimebeba sifa za zake na wazee wake,  sifa ambazo  huhama kwakurithisha kizazi chake, kwa mfano mwanaume kama atakuwa katika familia yake kulipatikana mtu mwenye ulemavu wa kuzaliwa, basi kuna uwezekano mkubwa naye akapata mtoto mwenye sifa hiyo, kwa mfano ulio wazi katika suala hili ni familia iliozaa watoto pacha kuwa katika watoto wa mama aua baba mwenye watoto mapacha, kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha, hivyo suala hili halikomei  kwa mapacha pekee katika kila sifa za mwanadamu.
Hivyo mafunzo ya Kiislamu yatutanabahisha   na kuzingatia mahala tunapokwenda kuoa au kuolewa kwaajili ya uboreshaji na kuleta wepesi wa kupatikana malezi bora kwa mtoto atakaye patikana kutokana na ndoa hiyo na kuipatia  jamii watoto wenye mwenendo mwema, hii ni hatua ya kwanza ya malezi bora ambayo mtukufu mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema:
(تخيروا لنطفكم، فان النساء يلدن اشباه أخوانهن واخواتهن)
chagueni kuoa katika familia njema, kwa hakika wanawake huzaa watoto wanaoshabihiana na kaka zao na dada zao  (kanzul umali, J16, k 295, hadithi 44557). Ndugu msomaji hili ni suala muhimu katika mwenendo na malezi ya mtoto kwani mtume (s.a.w.w) anawazindua wale walio na lengo la kuwapa malezi bora watoto zao kuwa wanapaswa kuzingatia kuwa wapi wanapaswa kuoa, kwa maana kwakufanya kwao hivyo wanaweza kurahisisha au kukwamisha upatikanaji wa malezi bora kwa vizazi vyao, ama wale ambao hawana nia ya kupata watoto na kushughulishwa na suala la malezi hawatakuwa na ulazima wa kufanya uchunguzi huu kwani uchunguzi huu ni kwaajili ya kurahisisha suala la malezi ambalo ni wadhifa wao kuwapatia watoto zao. Kula  
 Nukta muhimu katika hili ndugu wasomaji tunapaswa kuzingatia kuwa suala la kuchunguza kunako familia si wadhifa wa wanaume pekee wanapotaka kuoa bali mwanamke anapaswa kuchunguza familia ya mwanaume ili kufikia lengo lake mwenyezi Mungu anasema katika Qur`an:
)الْخَبِيثاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَ الْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثاتِ وَ الطَّيِّباتُ لِلطَّيِّبِينَ وَ الطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّباتِ أُولئِكَ مُبَرَّؤُنَ مِمَّا يَقُولُونَ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَ رِزْقٌ كَرِيم
‏  waovu wa kike ni kwaajili ya waovu wa kiume, na waovu wa kiume ni kwaajili ya waovu wa kike, pia wema wa kike ni kwaajili ya wema wa kiume na wema wa kiume ni kwaajili ya wema wa kike, hao huepushwa na yale wanayoyasema nao wana msamaha na riziki njema (surat nur 25)
 huu ndio mtazamo wa Uislamu katika kutengeza familia na kuandaa msingi sahihi ya malezi bora ya watoto, kwa maana mtu anapoona familia yake inakwenda kombo anapaswa kuchunguza wapi alipokosea na chanzo cha tatizo hilo.
Tunamuomba mwenyezi Mungu atuwezeshe kufuata mfumo wake ili tuweze kutii maamrisho yake na kupata jamii njema ambayo mtume mtukufu atafurahishwa nayo siku ya kiama.

Wako: MATENGA MKETO
 
     


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni