IMAMU WA KUMI NA MBILI

  • Habari NO : 256688

Jina:            Muhammad

Kuniya:    Abul Qasim

Lakabu:    Al-Mahdi, Al-Qa’im, al-Hujja, Sahib al-Amri Baba:         Hasan bin ‘Ali

Mama      Narjis (pia anajulikana kama Sausan, Sayqal) Kuzaliwa: 15 Sha’ban 255 A.H. huko Samarra, Iraq

Anaishi katika ghayb na atatokea kabla ya mwisho wa wakati

1.      KUZALIWA NA MAISHA YA MWANZONI

Imam Muhammad al-Mahdi (a.s.) alizaliwa mnamo tarehe 15 Sha’ban 255 A.H. (868 C.E.) huko Samarra na Bibi Narjis, mke wa Imam wa Kumi na Moja Imam   Hasan al-‘Askari (a.s.). Nasaba ya Bibi Narjis inarejea nyuma mpaka kwa Simon (Sham’un), mmoja wa wanafunzi wa Nabii ‘Isa (a.s.); na alikuwa akiheshimiwa sana na Bibi Hakima, dada yake Imam Ali an-Naqi (a.s.) na Kiongozi wa wanawake wa Bani Hashim.

Tangu taarifa juu ya kutazamiwa kuzaliwa kwa Mahdi, yule masihi atakaekomesha dhulma na ukorofi zilipoenea sana, Bani ‘Abbas walikuwa wanaiangalia kwa karibu sana familia ya Ahlul Bayt (a.s.). Hali haikuwa tofauti na zile siku kabla ya kuzaliwa Mtume Musa (a.s.) wakati Pharoah (Firauni) alipotoa amri kwamba watoto wote wa kiume wa wana wa Israeli wauawe. Kama vile kuzaliwa kwa Musa kulivyofichwa kwa watu kwa nguvu zake Allah, kuzaliwa kwa Muhammad Al-mahdi pia kufichwa kwa watu.

                    Kwa miaka mitano,Imam Al-mahdi Aliishi chini ya malezi ya

upendo ya baba yake. Alikuwa akionwa na watu wa familia tu na

wachache waliochaguliwa na baba yake. Hii yote ilifanywa ili kumkinga na wapelelezi wa Bani ‘Abbas. Baadhi ya wale waliomuona Imam wakati huo wametajwa hapa chini:

1.  Bibi Hakima, shangazi yake Imam Hasan al-‘Askari (a.s.)

2.  Nasim, mtumishi wa Imam al-‘Askari

3.  Muhammad bin ‘Uthman al-‘Amri

4.  Husayn bin al-Hasan al-‘Alawi

5.  Ja’far bin Muhammad bin Malik na kikundi chake

6.  Ahmad bin Ishaq

Hapa tutasimulia tu lile tukio ambamo Ahmad bin Ishaq alimuona Imam al-Mahdi. Ahmad, Shia maarufu wa wakati huo, wakati mmoja alimtembelea Imam Hasan al-‘Askari (a.s.) na akataka kumuuliza kuhusu mrithi wake. Kabla hata Ahmad hajauliza swali lake, Imam akasema, “Ewe Ahmad! Kutoka siku Alipomuumba Adam, Allah hajaiacha ardhi bila ya mwakilishi (Hujjat au Hoja), wala hataiacha bila muwakilishi mpaka siku ya hukumu. Ni kwa sababu ya Hoja hiyo kwamba Allah anaikinga adhabu kwa watu, ananyeshesha mvua na kuotesha baraka kutoka ardhini”.

Ahmad: “Ewe mtoto wa Mtume! Ni nani mrithi na Imam baada yako?”.

Imam Hasan al-‘Askari mara moja akaingia ndani ya nyumba na akarudi na kijana wa miaka mitatu mikononi mwake, “Ewe Ahmad bin Ishaq, kama hungekuwa mwenye heshma mbele ya Allah na wawakilishi wake, nisingemuonyesha kijana wangu huyu kwako. Jina lake na Kuniya yake ni sawasawa na ile ya Mtume; huyu ndie ambae ataijaza dunia na haki na usawa kama vile tu itakavyokuwa imejazwa na dhulma na ukorofi.

 

 


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni