Ethiopia yateua timu kwa ajili ya mazungumzo ya amani na waasi wa Tigray Nairobi
Serikali ya Ethiopia imewataja wajumbe saba wa mazungumzo ya amani na waasi wa Tigray. Timu hiyo ilitangazwa baada ya kamati Kuu ya Utendaji ya chama tawala cha Prosperity Party kufanya mikutano kuhusu mgogoro huo katika eneo la kaskazini mwa nchi.