2 Desemba 2025 - 15:18
Kikao cha Papa na Naibu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon mjini Beirut

Naibu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na Papa, alisisitiza kwamba utamaduni wa kiroho wa Uislamu umejengwa juu ya misingi ya usawa na heshima ya utu wa binadamu, na akakumbusha kwamba mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) na Imam Ali (a.s) yanabainisha umuhimu wa udugu wa kibinadamu na maelewano kati ya watu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Leo hii, tarehe 2 Desemba 2025, katika kongamano la mazungumzo ya kidini lililofanyika katika Uwanja wa Mashahidi (Midan al-Shuhada) katikati ya Beirut, Sheikh Ali al-Khatib, Naibu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon, alikutana na Papa Leoni wa Kumi na Nne, na kusisitiza misingi ya pamoja ya kibinadamu na kidini kati ya Waislamu na Wakristo.

Sheikh al-Khatib alimshukuru Papa kwa safari yake nchini Lebanon katika hali ngumu za sasa, na akaitaja ziara hiyo kuwa ni fursa muhimu ya kuimarisha umoja wa kitaifa.

Akimrejelea tena misingi ya kiroho ya Uislamu, alisisitiza kuwa dini hii inahimiza usawa na kuheshimu hadhi ya mwanadamu. Aidha, alikumbusha kuwa mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) na Imam Ali (a.s) yameweka wazi thamani ya udugu wa kibinadamu na kuishi pamoja kwa amani.

Alisema kwamba tofauti ni jambo la kawaida, lakini mahusiano ya wanadamu yanapaswa kujengwa juu ya mazungumzo, kuelewana, na kushirikiana—si juu ya vita vinavyopandikizwa kwa jina la dini.

Mwanazuoni huyo wa Kishia pia aligusia kuendelea kwa uvamizi wa Israel, akibainisha kuwa Lebanon, kutokana na kukosekana kwa serikali madhubuti, imelazimika kujilinda yenyewe.

Alimwomba Papa kutumia nafasi na uwezo wa taasisi za kimataifa ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kusaidia Lebanon kupita kwenye misururu ya migogoro iliyoikumba, hususan madhara ya uvamizi wa Israel.

Your Comment

You are replying to: .
captcha