9 Juni 2026 - 22:43
Kamanda wa Majeshi ya Ardhi ya Iran: Tumejiandaa Kujibu kwa Uamuzi Vitisho Vyovyote

Kamanda wa Majeshi ya Ardhi ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Ali Jahanshahi, amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vilivyoko mpakani viko katika utayari kamili wa kioperesheni na vimejiandaa kukabiliana kwa uthabiti na vitisho vyovyote vinavyoweza kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- , Kamanda wa Majeshi ya Ardhi ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ali Jahanshahi, amesisitiza kuwa vikosi vya nchi hiyo vilivyoko katika maeneo ya mipaka viko katika hali ya juu ya utayari wa kiusalama na kioperesheni.

Brigedia Jenerali Jahanshahi alitoa kauli hiyo alipokuwa akikagua vikosi vya operesheni katika Brigedi ya 71 ya askari wa miguu wa mekaniki “Abu Dhar” iliyopo katika ukanda wa mpaka wa magharibi wa nchi, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa mipaka ya taifa.

Ameeleza kuwa wanajeshi wa Majeshi ya Ardhi ya Iran wana uelewa wa kina wa hali ya usalama ya nchi na wako tayari kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kujibu kwa nguvu na uamuzi dhidi ya vitisho vyovyote vinavyoweza kutokea.

Aidha, amebainisha kuwa mafunzo ya mara kwa mara, utayari wa hali ya juu na ufuatiliaji wa karibu wa hali ya mipaka ni miongoni mwa sababu zinazowezesha vikosi hivyo kubaki imara katika kulinda mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kauli hiyo inakuja katika mazingira ya kuendelea kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya kikanda, ambapo mataifa mbalimbali yanaimarisha ulinzi na uwezo wao wa kijeshi kwa lengo la kukabiliana na vitisho vinavyoweza kujitokeza.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha