13 Agosti 2026 - 22:14
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Jaribio lolote la kuupuuza suala la Palestina linakataliwa

Iran imelaani vikali madai ya Waziri Mkuu wa Israel kuhusu umiliki wa kudumu wa Milima ya Golan na kukataa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina, ikisisitiza kuwa hatua za kikoloni haziwezi kubadilisha ukweli wa kihistoria na kisheria.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel kuhusu madai ya umiliki wa kudumu wa Milima ya Golan na kupinga kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.

Katika taarifa iliyotolewa leo Alhamisi kuhusu kuendelea kwa sera za upanuzi za Israel, Wizara hiyo imesema hatua za kikoloni zinazofanywa na kile ilichokiita chombo kinachokalia na kutwaa ardhi kwa mabavu haziwezi kubadilisha ukweli wa kihistoria na kisheria.

Taarifa hiyo imesema kiongozi wa utawala unaotawala katika ardhi ya Palestina inayokaliwa hana nafasi ya kutoa maoni kuhusu kuundwa kwa Dola huru ya Palestina, kwa kuwa ardhi ya Palestina ni mali ya wananchi wa Palestina.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeongeza kuwa mitazamo ya kibaguzi ya Israel, ambayo Iran inaituhumu kwa kufanya mauaji ya halaiki, haiwezi kubadilisha uhalisia huo wala kuondoa haki ya watu wa Palestina ya kuamua mustakabali wa nchi yao.

Kuhusu Milima ya Golan, taarifa hiyo imesisitiza kuwa eneo hilo ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya ardhi ya Syria, na kwamba hatua za kikoloni za Israel haziwezi kubadilisha ukweli huo wa kihistoria na kisheria.

Iran imeendelea kusisitiza kuwa masuala yanayohusu ardhi ya Palestina na haki za wananchi wa Palestina hayawezi kupuuzwa au kuondolewa katika ajenda ya kisiasa na kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha