Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Chanzo cha kijeshi nchini Yemen kimetangaza kuwa, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, vikosi vya kijeshi vya Yemen vimefanikiwa kulenga kituo cha Aramco huko Najran, Saudi Arabia, kwa kutumia ndege isiyo na rubani (droni), na kudai kuwa operesheni hiyo imefanikiwa kufikia lengo lake.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, shambulio hilo limefanyika kama jibu dhidi ya kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukaji wa mamlaka ya Yemen na ndege za kijeshi za Saudi Arabia, pamoja na kuvuka anga la kaskazini-mashariki mwa Mkoa wa Saada.
Maoni yako