Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– DAR ES SALAAM, Tanzania: Kituo cha Noor Centre Dar es Salaam kimefanikiwa kuandaa kikao maalum cha kielimu na kidini kilichofanyika tarehe 27 Agosti 2026, kwa lengo la kujadili nafasi na umuhimu wa ujumbe wa Mtume Muhammad (saww) katika ulimwengu wa kisasa.
Kikao hicho kiliongozwa na Sheikh Ali Asad Esmail, ambaye alitoa mada yenye kichwa “Utume wa Mtume (saww) Katika Dunia ya Kisasa”, akieleza umuhimu wa ujumbe wa Mtume Muhammad (saww) katika kuwaongoza wanadamu na kujenga jamii yenye maadili, amani na mshikamano.
Programu hiyo ilihudhuriwa na waumini na wadau mbalimbali waliokusanyika kwa ajili ya kunufaika na mawaidha na mafundisho yaliyotolewa katika kikao hicho.
Waandaaji wamemshukuru Allah (SWT) kwa kufanikisha programu hiyo, huku wakiwaombea malipo mema wote waliohudhuria, kusaidia na kuchangia katika kufanikisha kikao hicho.
Aidha, wameendelea kumuomba Allah (SWT) ayakubali mema yaliyofanywa katika programu hiyo kwa kusema: “Allahumma taqabbal minna. Ameen.”
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kuendeleza elimu na ufahamu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na namna yanavyoweza kutumika katika kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa.
Maoni yako