Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohseni Ejei, Rais wa Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amefanya ziara katika hospitali moja mjini Tehran kumjulia hali Ayatollah Nouri Hamedani, mmoja wa Marjaa wakubwa wa kidini wa Kishia nchini Iran.
Katika ziara hiyo, kiongozi wa timu ya madaktari wanaomhudumia Ayatollah Nouri Hamedani alitoa taarifa kuhusu mwenendo wa matibabu yake.
Kiongozi huyo wa timu ya madaktari alieleza matumaini kwamba, kutokana na hali ya afya ya Ayatollah Nouri Hamadani kuendelea kuimarika, ataruhusiwa kutoka hospitalini hivi karibuni.
Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kumjulia hali mwanazuoni huyo mashuhuri na kufahamu maendeleo ya afya yake.
Maoni yako