?>

255 wauawa na mamia wajeruhiwa katika tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Afghanistan

255 wauawa na mamia wajeruhiwa katika tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Afghanistan

Watu wasiopungua 255 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuyakumba maeneo ya mbali kusini mashariki ya Afghanistan na nchi jirani ya Pakistan alfajiri ya kuamkia leo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Mkuu wa wizara inayoshughulikia majanga ya kimaumbile katika serikali ya Taliban Mohammad Nassim Haqqani amesema, vifo vingi zaidi vimetokea katika mkoa wa Paktika, ambako watu wapatao 100 wameuawa na wengine 250 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Haqqani watu wengine 25 wamefariki katika mji wa Khost na watano katika mkoa wa Nangarhar na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa ili kubaini kama kuna maafa zaidi yametokea kutokana na zilzala hiyo.

Picha katika vyombo vya habari vya Afghanistan zimeonyesha jinsi nyumba zilivyogeuzwa vifusi.

Hadi sasa bado hazijatolewa ripoti kuhusu hasara au maafa yaliyosababishwa na tetemeko hilo nchini Pakistan.

Idara ya Jiolojia ya Marekani imeripoti mapema leo kuwa, zilzala hiyo iliyokuwa na ukubwa wa 6.1 kwa kipimo cha rishta ilipiga eneo la kilomita 44 kutoka mji wa Khost karibu na mpaka wa Pakistan na katika kina cha kiomita 51.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*