?>

Abdollahian: Haipasi kutumia mabavu na mtutu wa bunduki kutatua migogoro

Abdollahian: Haipasi kutumia mabavu na mtutu wa bunduki kutatua migogoro

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, haipasi kutumia njia ya mabavu na ya kijeshi katika kuyapatia ufumbuzi matatizo na migogoro mbalimbali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo pambizoni mwa mazungumzo yake na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani na kubainisha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa na nafasi ya kimhimili, muhimu na ya kimsingi katika masuala ya Asia Magharibi.

Kadhalika Amir-Abdollahian amesisitiza kuwa, siku zote Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa upande mzuri wa matukio ya eneo, iwe ni katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh au mazungumzo.

Vilevile Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, daima Tehran imekuwa ikitangaza utayari wake wa kufanya mazungumzo yanayolenga kuweko ushirikiano katika eneo la Ghuba ya Uajemi na imekuwa ikitoa mipango na mapendekezo katika uwanja huo.

Aidha akiwa Doha mji mkuu wa Qatar hapo jana, Amir-Abdollahian alikutana na kufanya mazungumzo na Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kusisitiza kuwa Iran itaendelea kuunga mkono haki za watu wa Palestina wanaopambana na utawala ghasibu wa Israel.

Katika mazungumzo hayo, Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ameishukuru kwa dhati tena Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na uungaji mkono wake kwa mapambano ya taifa la Palestina dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, kama ambavyo, ametoa wito kwa nchi zote za Kiislamu, Kiarabu na jamii ya kimataifa kwa ujumla kuchukua hatua za kivitendo za kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*