?>

Al Azhar yaonya kuhusu madhara ya kushambuliwa nyumba za Waislamu nchini India

Al Azhar yaonya kuhusu madhara ya kushambuliwa nyumba za Waislamu nchini India

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al Azhar cha nchini Misri kimelaani jinai za Wahindu za kushambulia nyumba za Waislamu nchini India na kuonya kuhusu madhara ya jinai hizo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Sputnik limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Chuo Kikuu cha al Azhar kimesema katika taarifa yake kuwa, kinalaani kwa nguvu zote jinai zinazofanywa na askari wa India za kuvunja nyumba za raia Waislamu wa nchi hiyo.

Jinai hizo mpya za askari wa India zinafanyika wakati huu ambapo Umma wa Kiislamu bado unauguza majeraha ya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW kulikofanya hivi karibuni na maafisa wawili wa ngazi za juu wa chama tawala cha BJP cha nchini India. Waislamu wa kona mbalimbali za dunia wamefanya maandamano ya kulaani vikali utovu wa adabu huo uliofanywa na Wahindu hao dhidi ya bwana Mtume Muhammad SAW.

Chama tawala cha BJP huko India kilichukua hatua ya kupumbaza watu ya kutangaza kuwafuta uanachama viongozi wake hao wawili waandamizi, lakini askari ambao wako chini ya serikali ya chama hicho hicho wanaendelea kukandamiza raia Waislamu bila ya kujali athari zake mbaya.

Chuo Kikuu cha al Azhar cha nchini Misri vile vile kimesema katika tamko lake hilo kwamba, kushambuliwa raia Waislamu wa India ni jinai, ni kitendo kisicho cha maadili na ni kinyume na tabia ya binadamu waliostaarabika. Vile vile kimesema, hatua hizo za askari wa India dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo zina maana ya kudharau hasira za Waislamu duniani na kuchezea shere sheria zote za kupinga uhalifu, kudhalilisha wengine na kuvunjia heshima imani na matukufu ya kidini na kimadhehebu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*