?>

Al Houthi: UN inashindwa hata kutatua mgogoro mmoja wa mafuta itaviweza vita vya Yemen?

Al Houthi: UN inashindwa hata kutatua mgogoro mmoja wa mafuta itaviweza vita vya Yemen?

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ameilalamikia vikali jamii ya kimataifa kwa kutojali wala kushughuishwa na maafa ya kibinadamu wanayofanyiwa wananchi wa Yemen na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia na kusisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa unashindwa hata kutatua mgogoro mmoja tu wa mafuta, utaweza kweli kutatua mgogoro wa vita vya Yemen?

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: limeripoti habari hiyo leo Alkhamisi na kumnukuu Muhammad Ali al Houthi akisema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina uwezo wa kutatua mgogoro wa Yemen.

Vile vile amesema, madai yanayotolewa na maadui wa taifa la Yemen hayana msingi wowote na ni ndoto walizokuwa nazo wavamizi wa nchi hiyo, amma cha kusikitisha ni kuwa, hadi hivi sasa msimamo wa jamii ya kimataifa kuhusu maafa makubwa ya kibinadamu yanayosababishwa na wavamizi wa Yemen hayajawasaidia chochote wananchi wa nchi hiyo.

Huku hayo yakiripotiwa, Umoja wa Mataifa umesema kuwa, unahitaji dola bilioni 3.9 za kuwasaidia mamilioni ya wananchi wa Yemen walioathiriwa vibaya na vita.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Ramesh Rajasingham, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya misaada ya kibinadamu akitangaza habari hiyo jana Jumatano na kuongeza kuwa, kikwazo kikubwa kinachokwamisha kupatiwa misaada watu takriban milioni 16 wa Yemen walioathiriwa vibaya na vita, ni kukosekana vyanzo vya fedha.

Naye Hisham Sharaf, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen siku chache ziizopita alisema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kutekeleza jukumu lake la kulilinda taifa la Yemen mbele ya jinai za utawala wa kiimla wa Saudia na wavamizi wenzake.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*