?>

Al-Mushiri: Haftar ni tishio kwa uchaguzi mkuu wa Libya

Al-Mushiri: Haftar ni tishio kwa uchaguzi mkuu wa Libya

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Libya amesema kutosalimu amri kwa kamanda wa linalojiita jeshi la taifa mbele ya mamlaka au sheria yoyote ni tishio kwa chaguzi zijao za Bunge na Rais.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Khaled al-Mushiri ameyasema hayo katika mazungumzo yake na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya. Ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na harakati za wapiganaji wa linalojiita jeshi la taifa linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar dhidi ya uchaguzi ujao na kusema kuwa, suala hilo linaonesha kuwa, serikali ya sasa ya Libya haijaweza kueneza mamlaka yake nchini kote na kwamba Haftar hatii mamlaka ya serikali ya mpito; suala ambalo amesisitiza kuwa ni tishio kwa mchakato wa kuitishwa uchaguzi salama na wa wazi. 

Wiki iliyopiita wapiganaji wa Khalifa Haftar walizuia kikao cha wajumbe wa serikali ya mpito ya Libya katika mji wa Benghazi mashariki mwa nchi hiyo. 

Serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Abdulhamid al-Dabaiba na Baraza la Urais chini ya uongozi wa Mohamed al-Menfi tarehe 16 mwezi wa Machi mwaka huu ilishika rasmi hatamu za kuiongoza nchi hiyo na kutayarisha mazingira ya kuitishwa chaguzi za Bunge na Rais mwishoni mwaka huu wa 2021. 

Kabla ya kuundwa serikali ya mpito ya umoja wa kifaifa, Libya ilikuwa ikiongozwa na serikali mbili tofauti; ile ya mashariki mwa nchi chini ya uongozi wa jenerali muasi, Khalifa Haftar na serikali ya Tripoti iliyokuwa ikiungwa mkono na Umoja wa Mataifa.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*