?>

Al Zahar: Jinai za Israel ni matunda ya kuanzishwa uhusiano baina yake na nchi za Kiarabu

Al Zahar: Jinai za Israel ni matunda ya kuanzishwa uhusiano baina yake na nchi za Kiarabu

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, jinai unazofanya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina ni matunda ya hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia.

(ABNA24.com) Mahmoud Al Zahar ameyasema hayo katika mahojiano na tovuti ya Al Arabiyyul-Jadid na kuongeza kwamba: Kwa kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Kiarabu, utawala huo haramu umepata baraka kamili za kufanya jinai na kushadidisha mashambulio dhidi ya Wapalestina, kukanyaga haki zao za kitaifa na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Mjumbe huyo mwandamizi wa Hamas ameashiria jinai ya karibuni ya utawala wa Kizayuni ya kumuua shahidi kijana mmoja wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza na kisha kuivunjia heshima maiti yake na akasema: Kitendo hicho kimedhihirisha sura halisi ya utawala ghasibu wa Israel huku nchi nyingi duniani zikiendelea kupuuza na kufumbia macho jinai hizo.

Dakta Mahmoud Al Zahar amebainisha kuwa, mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' ni sawa na kibali cha kuuruhusu utawala wa Kizayuni ufanye jinai zaidi na hujuma dhidi ya Wapalestina bila kupingwa na nchi za Kiarabu na za Ulaya au hata mashirika ya kimataifa na asasi za kisheria na za huduma za kibinadamu.

Katika kitendo cha kishenzi na cha kinyama walichofanya siku ya Jumapili baada ya kumuua shahidi Muhammad An-Naim kijana wa Kipalestina kusini mwa Ukanda wa Gaza, askari wa utawala wa Kizayuni siku ya Jumapili waliiponda ponda pia kwa buldoza maiti ya shahidi huyo wa Muqawama.

...........
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni