?>

Amir-Abdollahian: Chokochoko za utawala wa Kizayuni lazima zitajibiwa

Amir-Abdollahian: Chokochoko za utawala wa Kizayuni lazima zitajibiwa

Katibu Mkuu wa Mkutano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina amesisitiza kuwa, chokochoko na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel hazitoachwa vivi hivi bila ya kujibiwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo jana kwa mnasaba wa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Amesema hayo wakati alipoonana na Khaled al Qaddumi, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Tehran na kwa mara nyingine amesisita kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono bila ya woga ukombozi wa Quds na Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Katika mazungumzo hayo, Amir-Abdollahian amegusia matukio ya eneo hili na ya ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kusema, chokochoko na jinai za utawala wa Kizayuni kamwe haziwezi kuachwa zipite hivi hivi bila ya kujibiwa na kwamba kambi ya muqawama itandelea kukabiliana na jeuri na ujuba wowote ule wa Wazayuni kwa nguvu zote kuliko huko nyuma.

Vile vile amesema, leo hii muqawama wa Palestina uko imara zaidi na una taathira kubwa zaidi kisiasa na katika medani za mapambano, kuliko wakati mwingine wowote wa huko nyuma.

Aidha amezilaumu vikali nchi za Kiarabu za Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Bahrain, Sudan na Morocco kwa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuhimiza umoja na mshikamano katika safu za Wapaelstina. 

Kwa upande wake, Khaled al Qaddumi, Mkuu wa Ofisi ya HAMAS mjini Tehran ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji wake mkubwa kwa taifa la Palestina na huku akishukuru ubunifu wa Imaam Khomeini wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds na kuimarisha ubunifu huo na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko pamoja na taifa linalodhulumiwa la Palestina na linahimili mashinikizo na vikwazo vya kila aina kwa ajili ya ukombozi wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*