?>

An-Nujabaa ya Iraq yawaambia Wapalestina: Tuko tayari kwa mapambano na utawala wa Kizayuni

An-Nujabaa ya Iraq yawaambia Wapalestina: Tuko tayari kwa mapambano na utawala wa Kizayuni

Katibu Mkuu wa Harakati ya An-Nujabaa ya Iraq amesisitiza katika ujumbe aliotuma kwa wananchi wa Palestina kuwa, vikosi vya harakati hiyo viko tayari kwa ajili ya kupambana na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akram al Kaabi, Katibu Mkuu wa Harakati ya An-Nujabaa ya Iraq ameeleza katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa twitter: "Tangu pale nyinyi mlipopigilia misumari ya 'Upanga wa Quds' kwenye jeneza la maghasibu, tungali tunafurahia ushindi huu na utetezi wa msikiti wa Al Aqsa. Wakati lengo tukufu, ushindi na ardhi yake ni moja, Baghdad ni Quds na Quds ni Baghdad. Adui naye ni mmoja tu, awe wa Kizayuni au wa Kimarekani."

Al Kaabi amesisitiza kwa kusema: "Tunatangaza kinagaubaga kwamba, sisi tuko pamoja na nyinyi bega kwa bega katika kulinda na kutetea matukufu ya Palestina. Tunaongejea mutupe ishara tu ili tujitokeze kwa damu na silaha. Kwa kila Muislamu na kwa kila mwanamuqawama, leo hii imeshabainika wazi kuwa piganio tukufu la Palestina ndio mtazamo wa umma wote wa Kiislamu na ndio muelekeo wa kila mpigania ukombozi na mwanamuqwama katika dunia hii."

Katibu Mkuu wa Harakati ya Nujabaa ya Iraq amebainisha pia kuwa, kwa miaka kadhaa sasa, wanajihadi wa harakati hiyo wanasubiri kupambana na maghasibu wa ardhi ya Palestina na wanangojea ifike siku ambapo mitutu ya bunduki iliyo chini ya mhimili wa Muqawama itakapoelekezwa kwa waistikbari wa Kizayuni wanaoikalia ardhi hiyo pamoja na Marekani inayowaunga mkono.../


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*