?>

Aprili pekee, Wapalestina 270 wamekamatwa na kuhamishwa baada kubomolewa nyumba zao

Aprili pekee, Wapalestina 270 wamekamatwa na kuhamishwa baada kubomolewa nyumba zao

Katika mwezi mmoja tu uliopita wa Aprili, askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wameshadidisha hujuma na mashambulio katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) na msikiti mtukufu wa Al Aqsa; na katika kipindi hicho wamewakamata na kuwahamisha katika nyumba zao Wapalestina zaidi ya 270.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kanali ya habari ya Meidanul-Quds imeripoti kuwa, katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na tangu siku 12 zilizopita, Wazayuni wamevamia eneo la Babul-a'muud na maeneo ya kandokando ya msikiti wa Al Aqsa na kuwashambulia Wapalestina walio katika hali ya Saumu kwa mabomu ya kutoa machozi, sambamba na kuwatusi na kuwapiga.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, walowezi zaidi ya 3,400 wa Kizayuni wamevamia msikiti wa Al Aqsa na lango la Babul-a'muud na kwamba hujuma zao zimeshtadi hasa katika mwezi huu wa Ramadhani.

Wapalestina wapatao 420 waliokuwa wamefunga wamejeruhiwa na makumi ya wengine wamekamatwa katika hujuma iliyofanywa na askari wa utawala haramu wa Israel wakishirikiana na walowezi wa Kizayuni dhidi ya eneo la Babul-a'muud.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*