?>

Araqchi: Kumefikiwa mapatano ya kuondoa aghalabu ya vikwazo dhidi ya Iran

Araqchi: Kumefikiwa mapatano ya kuondoa aghalabu ya vikwazo dhidi ya Iran

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kikao cha jana cha Tume ya Pamoja ya Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA na kusema kikao hicho kimefikia mwafaka kuhusu kuondolewa Iran vikwazo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Abbas Araqchi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo Jumamosi baada ya kumalizika duru nyingine ya kikao cha tume hiyo ya pamoja ya JCPOA huko Vienna Austria. Amesema pande husika zimeafikiana kuhusu kuondolewa vikwazo aghalabu ya watu na taasisi katika orodha ya vikwazo ya Marekani. Aidha amesema mazungumzo zaidi yatafanyika kuhakikisha kuwa vikwazo vyote vinaondolewa.

Kikao hicho kilihudhuriwa na ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wawakilishi wa kundi la 4+1 ambalo linaundwa na nchi za Ufaransa, Russia, China, Uingereza na Ujerumani pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*