Kusanbaratishwa kwa Shambulizi la kigaidi ndani ya uwanja utakao cheza Iran na Morocco

Kusanbaratishwa kwa Shambulizi la kigaidi ndani ya uwanja utakao cheza Iran na Morocco

Vyombo vya ulinzi na uslama vya Urusi vimesambaratisha shambulio la kigaidi liliopangwa kufanywa katika kiwanja cha mpira kiliopangwa kucheza timu ya Iran na Morocco nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yameandikwa na Gazeti la Asabah la Morocco na kusisitiza kua majeshi ulinzi na usalama ya Urusi, yamefanikiwa kusambaratisha shambulio la kigaidi liliopangwa kufanywa katika kiwanja cha mpira ambacho kilipangwa icheze timu ya Iran na Morocco.
Aidha Gazeti hilo limeendelea kusema kuwa majeshi ya Urusi miezi kadhaa iliopita limewatuhumu na kuwatia mbaroni watu 1400 kuwa wanafungamano na ushirikiano na vikundi vya kigaidi na kupanga mashambulizi ya kigaidi nchini humu, ambapo watuhumiwa hao ni wananchi wa mataifa mbalimbali nchi ya Syria, Tunisia, Algeria na Netherlands.
Timu ya Taifa ya Iran na Morocco zilioingia katika kombe la Dunia la mwaka 2018 ambapo timu hizo zitacheza mnamo tarehe 15 Juni katika uwanja wa mpira wa Saint Petersburg nchini Urusi.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky