?>

Asilimia 17 ya Wamarekani hawaamini kabisa kwamba kuna Mungu

Asilimia 17 ya Wamarekani hawaamini kabisa kwamba kuna Mungu

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanyw ana ttaasisi ya Gallup ya nchini Marekani unaonesha kuwa, asilimia 17 ya wananchi wa nchi hiyo haamini kabisa kwamba kuna Mungu na hicho ni kiwango cha juu kabisha cha watu wasio na imani ya Mungu nchini Mrekani katika kipindi cha miaka 80 iliyopita.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Kwa mujibu wa New York Post, matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni uliofanywa na taasisi hiyo ya Gallup chini ya anwani "Matukufu, Imani na Itikadi" na ambao ulifanyika kuanzia tarehe 2 hadi 22 Mei 2022 yanaonesha kuwa, asilimia 81 ya Wamarekani wanaamini kuwa Mungu yupo, ingawa si wote wanaofuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, kiwango cha watu wasioamini kabisa kuweko Mungu nchini Marekani ni cha juu zaidi hivi sasa na hakijawahi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 1944.

Mwaka 1944 ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa taasisi ya Gallup kufanya uchunguzi wa maoni wa kuulizwa Wamarekani iwapo wanaamni kuwepo Mungu au la. Baada ya hapo ilifanya tena uchunguzi kama huo wa maoni mwaka 1947 na baadaye ilifanya uchunguzi kama huo mara mbili katika miongo ya 1950 na 1960. Katika miaka yote hiyo, asilimia 98 ya Wamarekani walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni walisema bila ya kutetereka kuwa wanaamini kuweko kwa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo baada ya kupita miongo 5 yaani mwaka 2011 wakati Gallup ilipofanya tena uchunguzi huo wa maoni ilishtuka kuona kuwa ni asilimia 92 ya Marekani ndio walioamini kuwa kuna Mungu.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba uchunguzi wa mwezi uliopita wa Mei umeonesha kuwa, ni asilimia 81 moja tu ya Wamarekani ndio wanaoamini kuweko kwa Mwenyezi Mungu hivi sasa. Gallup ilifanya pia uchunguzi kama huo wa maoni katika miaka ya 2013, 2014 na 2017.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*