?>

Asilimia 69 ya walowezi wa Kizayuni hawana imani na mustakbali wa Israel

Asilimia 69 ya walowezi wa Kizayuni hawana imani na mustakbali wa Israel

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimesambaza ripoti ambayo inaweza kuwa ni ya kutisha sana kwa walowezi wa Kizayuni. Ripoti hiyo inaonesha kuwa, idadi kubwa ya walowezi hao hawana imani na mustakbali wa utawala huo pandikizi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Gazeti la Hayom la utawala wa Kizayuni limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, asilimia 69 ya walowezi wa Kizayuni wana wasiwasi mkubwa kuhusu mustakbali wa Israel huku asilimia 75 ya Waarabu wa Israel wakisisitiza kuwa, Wazayuni hawana haki yoyote katika ardhi za Palestina.

Baada ya kupita miaka 100 ya Tangazo la Balfour na baada ya miaka 74 ya tangu kupandikizwa dola la Kizayuni la Israel katika kitovu cha nchi za Waislamu, hivi sasa wimbi la kukimbia walowezi wa Kizayuni limechukua nafasi ya msingi wa Tangazo la Balfour la kuwamimina Wazayuni hao katika ardhi za Palestina. 

Kwa mujibu wa kituo cha takwimu cha utawala wa Kizayuni, tangu mwaka 2009 wimbi la Mayahudi wanaohama kutoka ardhi za Palestina limechukua nafasi ya Mayahudi wanaohamia katika ardhi hizo. Hii ina maana kwamba idadi ya Mayahudi wanaokimbia katika ardhi hizo imeongezeka sana huku utamaduni wa kila Mzayuni kuwa na uraia wa nchi nyingine ukishamiri mno.

Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotangazwa na gazeti hilo la Kizayuni la Hayom yanaonesha pia kuwa, baada ya kupita mwaka mmoja wa operesheni ya "Upanga wa Quds" yaani vita baina ya utawala wa Kizayuni na wanamapambano wa Kiislamu wa Ukanda wa Ghaza, asilimia 66 ya Wazayuni hawana imani tena na jeshi la polisi la utawala wa Kizayuni.

Nacho kituo cha uchunguzi wa maoni cha Fenima cha Israel kimeripoti kuwa, asilimia 44 ya vijana wa utawala wa Kizayuni hawana imani wala mtazamo mzuri kuhusu mustakbali wa utawala huo pandikizi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*