?>

Askari polisi wa zamani wa Marekani: NYPD na FBI zilihusika na mauaji ya Malcolm X

Askari polisi wa zamani wa Marekani: NYPD na FBI zilihusika na mauaji ya Malcolm X

Aliyekuwa askari wa Polisi kuu ya Marekani ya jiji la New York NYPD amesema kabla ya kuaga dunia kwamba polisi hiyo na Polisi ya Upelelezi FBi zilihusika katika mauaji ya Februari 21, 1965 ya aliyekuwa kiongozi wa kupigania haki za kiraia nchini humo Malcolm X.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Barua iliyoandikwa na Raymond Wood, aliyekuwa askari polisi wa siri wa NYPD imeeleza kuwa, polisi hiyo na ile ya upelelezi FBI zilificha taarifa za ndani kuhusu mauaji ya Malcolm X na kuongeza kwamba, yeye Wood alitakiwa ajipenyeze ndani ya harakati za kupigania haki za kiraia na kuhakikisha walinzi wa timu ya usalama ya Malcolm X wanakamatwa muda mfupi kabla ya mauaji ya kiongozi huyo wa Wamarekani weusi.

"Nilishiriki kwenye vitendo vilivyopasa kulaaniwa, ambavyo nilikuja kubaini baadaye kwamba vilikuwa na madhara kwa watu weusi wenzangu. Vitendo vyangu, nilivyotumwa na Idara ya Polisi ya New York nilivifanya kwa sababu ya vitisho na hofu", imeeleza barua hiyo ya Raymond Wood iliyosomwa hadharani siku ya Jumamosi mbele ya waandishi wa habari na Reggie Wood ambaye ni mmoja wa jamaa zake.

Haijulikani ni lini Raymond Wood aliaga dunia, lakini kwa mujibu wa Reggie Wood alitaka barua yake hiyo isitolewe hadharani mpaka baada ya kifo chake kwa kuhofia kudhuriwa na mamlaka za serikali endapo angeibua madai hayo.

Barua hiyo imefafanua kuwa, utiaji nguvuni huo uliofanywa siku ya tarehe 21 Februari 1965 ulilenga kuhakikisha Malcolm X hawi na walinzi wa kudhamini usalama wake wakati anaingia kwenye ukumbi wa Audobon Ballroom ambako alihutubia siku hiyo.

Watoto watatu wa kike wa marehemu Malcolm X, familia ya Raymond Wood, pamoja na wakili wa kutetea haki za kiraia Ben Crump wamehimiza faili la mauaji ya kiongozi huyo wa Wamarekani weusi lifunguliwe upya haraka.

Malcolm X aliuliwa kwa kupigwa risasi ndani ya ukumbi wa Audobon Ballroom mjini New York na watu watatu waliotambuliwa kuwa ni wanachama wa harakati yake ya zamani ya Nation of Islam.

Watatu hao walipatikana na hatia ya mauaji na wakafungwa jela, lakini badaye waliachiwa huru kwa msamaha.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni