?>

Aswarullah: Muungano vamizi wa Yemen upate funzo kutokana na hali iliyomkumba Trump

Aswarullah: Muungano vamizi wa Yemen upate funzo kutokana na hali iliyomkumba Trump

Msemaji wa harakati ya wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia unapaswa ujifunze kutokana na hali iliyo nayo hivi sasa serikali ya Donald Trump huko Marekani hasa kwa vile wavamizi hao wa Yemen waliitumainia sana serikali hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya Almasirah imetangaza habari hiyo mapema leo Alkhamisi ikimnukuu Muhammad Abdus Salaam akisema kuwa, uungaji mkono wa Marekani hasa wakati wa utawala wa Donald Trump ndio uliochochea kuongezeka dhulma ya wavamizi na kuendelea kuzingirwa kila upande Yemen hadi leo hii.

Ameongeza kuwa, nchi zilizoivamia Yemen zinapaswa zikomeshe mara moja uvamizi wao kwani muungano huo "nusu mfu" hauna chochote kipya unachoweza kuwafanyia wananchi wa Yemen.

Jana Jumatano, Bunge la Marekani lilipasisha muswada wa kumburuza bungeni hapo kwa mara ya pili, rais wa nchi hiyo, Donald Trump kutokana na kuwachochea wafuasi wake wavamie na kufanya mauaji na uharibifu ndani ya jengo la Congress.

Wavamizi wa Yemen hasa Saudia na Imarati walikuwa na matumaini makubwa ya kufikia malengo yao haramu huko Yemen kwa msaada wa serikali ya Donald Trump. Hata hivyo serikali hiyo imebakiwa na siku chache tu hadi kukata roho. Ikumbukwe pia kuwa tangu wavamizi walipoanzisha mashambulio ya kila upande dhidi ya wananchi maskini wa Yemen, mwezi Machi 2015, hadi hivi sasa, muda wote Marekani imekuwa ikiunga mkono kwa hali na mali jinai za wavamizi hao.

Hadi hivi sasa zaidi ya wananchi 16,000 wa Yemen wameshauawa, makumi ya maelfu wamejeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi kutokana na uvamizi huo unaoongozwa na Saudi Arabia.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni