?>

Balozi wa Kenya mjini Tehran: Iran ni kigezo mwafaka kwa ajili ya ustawi wa Kenya

Balozi wa Kenya mjini Tehran: Iran ni kigezo mwafaka kwa ajili ya ustawi wa Kenya

Balozi wa Jamhuri ya Kenya mjini Tehran amesema kuwa, licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kukabiliwa na matatizo hususan vita vya kujihami vya miaka minane na vikwazo, lakini ni kigezo mwafaka kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kenya.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Balozi Joshua Gatimu amesema hayo katika mazungumzo yake na Meya wa mji wa Kashan ulioko kusini mwa Tehran ambapo ameashiria mashirikiano ya kiutamaduni ya Iran na Kenya na kueleza kwamba, kuhifadhiwa majengo ya kihistoria katika mji wa Kashan ni hatua chanya.

Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuweko mabadilishano ya uzoefu na mji wa Kashan na kueleza kwamba, kuna nyanja nyingi za ushirikiano ambazo zinaweza kuandaa uwanja na mazingira ya hili.

Balozi Gatimu amesema kuwa, huko kale Kenya ilikuwa mwenyeji wa kaumu mbalimbali za Kiirani na hili ni jambo ambalo limeongeza mashirikiano ya kiutamaduni baina ya nchi mbili hizi.

Kadhalika balozi wa Kenya mjini Tehran ameashiria usafi na uzuri wa mji wa Kashani na kueleza kwamba, kuna miji nchini Kenya ambayo ina sifa kama mji huu tofauti ikiwa ni kwamba, katika miiji hiyo ya Kenya kuna mvua nyingi.

Kwa upande wake, Hassan Bakhshandeh Meya wa mji wa Kashan amesisitiza juu ya utendaji wa uongozi wa miji kwa ajili ya kuimarisha udiplomasia wa miji na maeneo mbalimbali ya dunia hususan katika miji ambayo ina mshabaha wa kiutamaduni, kijamii, kijiografia na kiuchumi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*