?>

Balozi wa Palestina UN: Utawala wa Kizayuni ndio unaohusika na mauaji ya Shahidi Abu Akleh

Balozi wa Palestina UN: Utawala wa Kizayuni ndio unaohusika na mauaji ya Shahidi Abu Akleh

Balozi wa Palestina Umoja wa Mataifa amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio unaohusika na mauaji ya Shahidi Shireen Abu Akleh na akasisitiza kwamba, hawaukubali uchunguzi utakaofanywa na "maafisa wa utawala ghasibu wa Israel" kuhusu mauaji hayo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Alfajiri ya kuamkia Jumatano ya jana ya tarehe 11 Mei, askari wa utawala wa Kizayuni walimuua shahidi kwa kumpiga risasi ya uso Shireen Abu Akleh, ripota mwenye umri wa miaka 51 wa televisheni ya Aljazeera, wakati alipokuwa akiripoti habari za matukio ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Jenin na wakamjeruhi pia kwa risasi Ali As-Samudi, mwandishi wa gazeti la Palestina la Al-Quds.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Riyadh al-Mansour, balozi wa Palestina Umoja wa Mataifa amewaeleza waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja huo mjini New York kwamba, hawakubali uchunguzi wa watu ambao ndio wahalifu waliohusika kumuua shahidi Abu Akleh.

Al-Mansour amesisitiza kuwa, uchunguzi wa Israel hauaminiki na ni wa kubuni na ametaka ufanyike uchunguzi wa taasisi za kimataifa zinazoaminika.

Utawala katili wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umeshawatia nguvuni, kuwajeruhi na au kuwaua shahidi mamia ya wanahabari.

Kamati ya kuunga mkono waandishi wa habari wa Kipalestina ilitangaza hivi karibuni kuwa, lengo la utawala wa Kizayuni la kuchukua hatua za kiuadui dhidi ya wanahabari ni kuzuia kufichuliwa jinai ambazo utawala huo haramu unawatendea wananchi madhulumu wa Palestina.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*