?>

Baraza la Usalama la UN launga mkono suala la kuundwa nchi huru ya Palestina

Baraza la Usalama la UN launga mkono suala la kuundwa nchi huru ya Palestina

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza uungaji mkono wake kamili kwa suala la kuundwa nchi huru ya Palestina na kuendelezwa "mazungumzo yenye itibari" baina ya pande mbili.

(ABNA24.com) Taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao imepasishwa na wanachama wote wa baraza hilo imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na ukatili unaendelea kufanywa dhidi ya raia wa Palestina.

Taarifa hiyo pia imeashiria hatua zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kujenga vitongoji vipya vya walowezi huko Quds na kuzitaka pande zote kujiepusha na hatua yoyote inayozuia jitihada za kuimarisha amani ya kiadilifu, ya pande zote na ya kudumu.

Awali Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell alisema katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Riyadh al-Maliki kwamba umoja huo unaunga mkono suala la kuundwa nchi huru ya Palestina.

Malalamiko dhidi ya siasa na sera za kikatili za utawala wa Kizayuni wa Israel yameongezeka sana hususan baada ya kuwekwa wazi vipengee vya mpango uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani uliopewa jina la Muamala wa Karne uliozinduliwa White House tarehe 28 mwezi uliopita wa Januari.

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni, wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.

...........
340 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni