?>

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lataka hitilafu za Somalia zitatuliwe kwa njia za amani

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lataka hitilafu za Somalia zitatuliwe kwa njia za amani

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi limezungumzia matukio ya vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kutoa wito wa kupatiwa ufumbuzi hitilafu zinazoikabili nchi hiyo kwa njia za amani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Nayef bin Falah Al-Hajraf, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi amezitaka pande zinazozozana nchini Somalia kudumisha amani na utulivu na kuangalia uwezekano wa kuzipatia ufumbuzi hitilafu hizo kupitia mazungumzo na njia za amani.

Amesisitiza kuwa, mazungumzo na kufikiwa makubaliano ya kisiasa, ni jambo ambalo litaimarisha amani na ustawi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Alkhamisi iliyopita, milio mikubwa ya risasi na miripuko ilizuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wakati vikosi vya usalama vilipopambana na waandamanaji wenye hasira kutokana na kucheleweshwa uchaguzi.

Machafuko hayo yamejiri baada ya wiki kadhaa za mivutano na hali ya wasiwasi juu ya kufanyika uchaguzi uliocheleweshwa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Muungano wa wagombea wa upinzani nchini Somalia unamtaka Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kwa jina lake la utani la Farmaajo ang'atuke madarakani baada ya muhula wake wa urais kumalizika Februari 8.

Serikali ya Somalia imeikosoa Imarati kutokana na kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Mogadishu.

Waziri wa Habari wa Somalia ambaye alikuwa akijibu taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Imarati kuhusiana na yanayojiri ndani ya Somalia amesema kuwa, Abu Dhabi imeamua kukanyaga kanuni za kidiplomasia na kuwaunga mkono wapinzani wa Kisomali. Osman Abokor Dube ameitaka Imarati iombe radhi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni