?>

Boris Johnson akabiliwa na tuhuma za kadhia ya kurundikwa maiti za corona mahospitalini

Boris Johnson akabiliwa na tuhuma za kadhia ya kurundikwa maiti za corona mahospitalini

Viongozi wa vyama vya siasa Uingereza wamemtuhumu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Boris Johnson kuwa ni kidhabi na amesema uongo katika matamshi yake ya karibuni kuhusiana na kadhia ya kurundikwa maiti za maelfu ya wagonjwa wa corona katika majumba ya kuhifadhia maiti.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Jumatano ya jana Boris Johnson alikanusha tuhuma zinazohusiana na kadhia hiyo katika kikao cha maswali na majibu cha Bunge la Uingereza.

Gazeti la Independent limeandika kuwa, kiongozii wa chama Leba Keir Starmer, amesema katika kikako cha Bunge kwamba kama itabainika kuwa Boris Johnson amesema uongo katika matamshi yake kuhusiana na kadhia ya "kurundikwa maelfu ya maiti za wahanga wa corona", basi itampasa ajiuzulu. 

Imenukuliwa kuwa mwezi Oktoba mwaka jana Boris Johnson alisema kuwa, anafadhilisha kurundika maiti za maelfu ya wahanga wa corona kwenye majumba ya kuhifadhia maiti kuliko kutangaza duru nyingine ya sheria za karantini. 

Hivi karibuni pia gazeti la Daily Mail liliripoti kuwa, mwezi Oktoba mwaka jana Waziri Mkuu wa Uingereza alisema akiwa ofisini kwake Mtaa wa Downing kwamba: "Hakuna karantini nyingine malu'uni, wacha maelfu ya maiti zirundikane kwenye majumba ya kuhifadhia maiti."

Hadi sasa maafisa kadhaa wamethibitisha kuwa Boris Johnson ametoa matamshi hayo ambayo yeye mwenyewe ameyakana. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*