?>

Brigedi za al-Qassam: Tutatoa jibu kali kwa Israel endapo itathubutu kuua viongozi wa muqawama

Brigedi za al-Qassam: Tutatoa jibu kali kwa Israel endapo itathubutu kuua viongozi wa muqawama

Msemaji wa Brigedi za al Qassam ambazo ni tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameuonya utawala haramu wa Israel na hatua yoyote ya kijinga ya kuwaua viongozi wa muqawama.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Abu Ubeidah amesisitiza kuwa, kama utawala haramu wa Israel utafanya kosa la kijinga kwa kuwaua viongozi wa muqawama, basi utalipa gharama ya hilo kwa damu na kuangamia.

Msemaji wa Brigedi za al Qassam ambazo ni tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema, kwa kuzingatia vitisho vya adui muoga, tunamuonya adui na viongozi wake walioshindwa kwamba, madhara yoyote dhidi ya mwanajihadi Yahya Sinwar au kiongozi mwingine yeyote yule wa muqawama kutakuwa na maana ya kutangaza zilzala na mtetemeko wa ardhi katika eneo.

Amesema kuwa, jibu la muqawama kwa hatua hiyo ya kijinga ya Israel litakuwa kubwa kiasi kwamba, adui ataona vita vya Saif al-Quds ambapo alipata pigo pia lilikuwa jambo la kawaida kabisa. 

Hivi karibuni Wapalestina walitekeleza operesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv ambapo wazayuni watatu waliangamizwa na wengine wanne wamejeruhiwa.

Maafisa wa Kizayuni wa Israel wamembebesha lawama za operesheni hiyo Yahya Sinwar ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na wametoa wito wa kuuawa kwake.

Katika hotuba yake kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwenye Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, Sinwar alipongeza operesheni za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*