?>

Chanjo ya corona ya Iran kuingia awamu ya pili ya majaribio kwa wanadamu

Chanjo ya corona ya Iran kuingia awamu ya pili ya majaribio kwa wanadamu

Kundi la utafiti wa chanjo ya virusi vya corona ya Iran inalojulikana kwa jina la 'COVO-Iran Barakat' limetangaza kuwa chanjo hiyo iko tayari kwa ajili ya awamu ya pili ya majaribio kwa wanadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mtaalamu anayesimamia awamu mbalimbali za majaribio ya chanjo ya virusi vya corona ya COVO-Iran Barakat, Minoo Mohraz amesema leo kwamba, matokeo ya majaribio ya chanjo hiyo ni mazuri sana na kuongeza kuwa, baada ya kukamilika kikamilifu zoezi la awamu ya kwanza, yumkini wiki ijayo kukaanza awamu ya pili na kuchunguza taathira zake kwa mwanadamu. 

Mohraz amesema kuwa licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi lakini Iran imeweza kutayarisha miundomsingi ya kutengeneza na kuzalisha chanjo hiyo ya virusi vya corona.

Afisa huyo wa taasisi ya utafiti wa chanjo amesema kuwa, kwa kutilia maanani mafanikio yaliyopatikana katika awamu za utafiti na awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya COVO-Iran Barakat kwa wanadamu, Iran itakuwa na uwezo wa kuzalisha dozi milioni kumi za chanjo ya corona ya COVO-Iran Barakat hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa machipuo.

Afisa huyo wa masuala ya utafiti na teknolojia wa Wizara ya Afya ya Iran ameongeza kuwa, chanjo ya corona ya Cuba ambayo imepangwa kuzalishwa kwa kushirikiana na Iran imekamilisha awamu ya kwanza na ya pili nchini Cuba na awamu ya tatu ya majaribio yake ambayo itashirikisha watu baina ya 30 hadi 40 elfu, itafanyika nchini Iran na Cuba kwa wakati mmoja.

Awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya virusi vya corona ya COVO-Iran Barakat inayotengenezwa na wataalamu wa Iran ilianza tarehe 29 Disemba kwa watu waliojitolea wenyewe kushiriki katika zoezi hilo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni