?>

China kukabiliana na uchokozi baada ya meli za kivita za Marekani kupita Taiwan

China kukabiliana na uchokozi baada ya meli za kivita za Marekani kupita Taiwan

China imeituhumu Marekani kuwa inahatarisha usalama na kuvuruga utulivu wa kieneo baada ya meli za kivita za Marekani kupita katika Lango Bahari la Taiwan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa Jeshi la China ametangaza Jumanne kuwa nchi yake itachukua hatua zote zinazohitajika kukabiliana na vitisho na uchokozi sambamba na kulinda mamlaka yake ya kujitawala.

Manowari hizi za Marekani zimepita katika eneo la Lango Bahari la Taiwan katika kile Marekani inachodai kuwa ni uhuru wa kupita katika Bahari ya Indo-Pasifiki.

Hayo yanajiri siku chache tu baada ya Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa China Xi Jinping kurushiana maneno makali kuhusu Taiwan wakati walipokutana katika mkutano nadra uliofanyika kwa njia ya intaneti.  Katika kikao hicho, Xi alimtahadahrisha Biden kuwa kuhimiza eneo la Taiwan lijitenge na China ni sawa na kucheza na moto.

China imekuwa ikikosoa harakati za kichochezi zinazofanywa na Marekani katika Lango Bahari la Taiwan na kueleza kwamba, kuweko manowari ya Marekani katika eneo hilo kunahatarisha amani na utulivu katika njia hiyo ya baharini ya maji ya kimataifa.

China imeonesha kivitendo kwamba, japokuwa imekubali kulegeza kamba mkabala wa Marekani katika masuala kama ya ushindani wa kiuchumi lakini haiko tayari hata kidogo kusalimu amri au kulegeza kamba mbele ya mashinikizo ya aina yotote katika masuala yanayohusiana na mamlaka na ardhi ya nchi hiyo ikiwemo kadhia ya Taiwan. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*