?>

China yaishambulia kwa maneno Marekani kwa kuchochea machafuko Afghanistan

China yaishambulia kwa maneno Marekani kwa kuchochea machafuko Afghanistan

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ametoa maneno makali dhidi ya Marekani na kusema kuwa, viongozi wa Washington ndio wanaopaswa kubeba lawama ya mgogoro wa hivi sasa wa Afghanistan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la Tasnim limemnukuu Wang Yi akisema hayo jana katika matamshi yake kuhusu Afghanistan na kuongeza kuwa, Marekani ndiyo iliyoitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro na kuisababishia serikali ya Afghanistan matatizo mengi. Hivyo viongozi wa Marekani hawawezi kujivua na lawama kupitia kuropoka hapa na pale kuhusu mgogoro wa Afghanistan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China vile vile amesema, wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai hawapaswi kuiruhusu Marekani iiongezee matatizo serikali ya Kabul.

Huku hayo yakiripotiwa, mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai wameelezea wasiwasi wao kutokana na matukio ya kiusalama ya Afghanistan na wamehimiza kuheshimiwa matakwa ya wananchi wa nchi hiyo.

Wanachama wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ni China, Kazakhstan, Russia, Tajikistan, Uzbekistan, India na Pakistan. Nchi za Iran, Afghanistan, Belarus na Mongolia ni wanachama watazamaji wa jumuiya hiyo.

Tangu miezi mwili nyuma, sambamba na Marekani kutangaza kuondoa wanajeshi wake huko Afghanistan, kundi la Taliban limezidisha mashambulio yake katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, badala ya kukaa katika meza ya mazungumzo na serikali ya Kabul. Hivi sasa wanajeshi wa serikali ya Afghanistan wanaendesha mapambano ya kukabiliana na kukomboa maeneo yaliyotekwa na kundi la Taliban. Maeneo mengi ya Afghanistan yametekwa na kundi la Taliban sasa hivi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*