?>

Corona imeua watu 150,000 Uingereza ndani ya mwezi mmoja

Corona imeua watu 150,000 Uingereza ndani ya mwezi mmoja

Watu 150,000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19 katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita nchini Uingereza, hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo vya maradhi hayo kuwahi kusajiliwa nchini humo tangu janga la Corona lishike kasi Machi 2020.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Takwimu za Wizara ya Afya ya Uingereza zinasema kuwa, jana Jumamosi pekee, watu wengine 313 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza nchini humo.

Wizara hiyo imesema, nchi hiyo imesajili ongezeko la asilimia 38.3 la idadi ya vifo vilivyotokana na maradhi hayo ndani ya juma moja lililopita, ikilinganishwa na wiki ya kabla yake.

Kamati ya Pamoja ya Chanjo ya Uingereza imewataka wanachi kupigwa chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, wakati huu ambapo spishi ya Omicron inasambaa kwa kasi si tu katika nchi hiyo ya Ulaya, bali kote duniani.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu za Taifa nchini Uingereza, ugonjwa wa Covid-19 umeshaua watu 174,000, lakini takwimu za mashirika huru zinaonesha kuwa, idadi ya vifo vya maradhi hayo ipo juu mno.

Uingereza inashikilia nafasi ya saba duniani kwa idadi kubwa ya vifo na maambukizo ya Corona, ikitanguliwa na Marekani, Brazil, India, Russia, Mexico na Peru.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*