?>

Dk Tedros Adhanom achaguliwa tena kwa muhula wa pili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO

Dk Tedros Adhanom achaguliwa tena kwa muhula wa pili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO

Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) jana Jumanne zilithibitisha kuchaguliwa tena Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa kwa kipindi kingine cha pili.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kuchaguliwa tena kwa Dk Tedros raia wa Ethiopia, kumethibitishwa wakati wa Mkutano wa 75 wa Afya Ulimwenguni huko Geneva Uswisi.

Tedros aliteuliwa Januari 2022 kama mgombea pekee wa nafasi hiyo na Bodi ya Utendaji ya WHO.

Mchakato huo ulianza kwa nchi wanachama kutakiwa Aprili 2021 kuwasilisha majina ya wagombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

"Ninashukuru sana uaminifu na imani ya nchi wanachama kwangu. Ninawashukuru wafanyikazi wote wa afya na wenzangu wa WHO kote ulimwenguni. Ninatazamia kuendelea na safari yetu kwa pamoja,” Dk Tedros ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuchaguliwa tena.

Mamlaka yake mapya yanaanza rasmi tarehe 16 Agosti 2022. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anaweza kuteuliwa tena mara ya pili, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za WHO.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*