?>

Ehud Barak: Yamkini Israel ikaangamia baada ya miaka 6

Ehud Barak: Yamkini Israel ikaangamia baada ya miaka 6

Waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel Ehud Barak amesema ana wasiwasi mkubwa kuwa yamkini utawala huo utaangamia kabla ya kuadhimisha mwaka wa 80 tokea uasisiwe.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika mahojiano na gazeti la Kiibrania la Yedioth Ahronoth, kamanda huyo wa zamani wa jeshi la Israel amesema wasiwasi wake unatokana na kuwa katika historia, Mayahudi hawajawahi kutawala zaidi ya miaka 80 na hivyo ametabiri kuwa utawala wa sasa wa Tel Aviv unaweza kuangamia.

Mwaka huu utawala bandia wa Israel umeadhimisha mwaka wa 74 tokea uasisiwe katika ardhi ya Wapalestina.  Ikumbukwe kuwa mwezi Mei mwaka 1948, utawala bandia wa Israel ulitangaza uwepo wake baada ya kufanya mauaji makubwa ya umati dhidi ya Wapalestina. Siku hii inajulikana kama Siku ya Nakba ua Maafa. Katika siku hii kulifanyika maangamizi ya kimbari ya Wapalestina 700,000 sambamba na kubomolewa zaidi ya miji na vijiji 675.

Ehud Barak akibainisha zaidi kuhusu kukaribia kuangamiza utawala bandia wa Israel amesema: "Katika historia ya Uyahudi, Mayahudi hawajawahi kutawala zaidi ya miaka 80 isipokuwa tu katika tawala mbili za kifalme za Dawud na Hasmonean, na katika vipindi hivyo viwili, tawala hizo zilianza kusambaratika katika muongo wa nane."

Waziri Mkuu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 80 amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ni uzoefu wa tatu katika historia ya Uyahudi na sasa unakaribia mwaka wa 80 tokea uundwe.

Barak amesema ana wasiwasi mkubwa kuwa laana ya muongo wa nane itaukumba utawala wa sasa wa Israel.

Matamshi hayo ya Barak yanakuja wakati ambapo uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa vijana wengi raia wa Israel hawana matumaini kuhusu mustakabali wa utawala huo haramu. Uchunguzi huo uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Fenima ya Israel na kuchapishwa katika gazeti la Kiibrania la Hayom wiki iliyopita ulibaini kuwa asilimia 33 ya vijana wa Israel wanatafakari kuhama ardhi za Palestina ambazo Israle inazikalia kwa mabavu.  Aidha wengine asilimia 44 wanaamini kuwa utawala wa Israel hauna mustakbali.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*