?>

Emmanuel Macron aapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili

Emmanuel Macron aapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo ameapishwa kwa ajili ya kuhudumu kwa muhula wa pili kufuatia ushindi wake alioupata katika uchaguzi wa hivi karibuni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Macron aliibuka na ushindi wa asilimia 58 mkabala na asilimia 42 ya mpinzani wake mkuu na mkongwe Marine Le Pen, kimsingi kiongozi huyo ni mwakilishi wa asilimia 38 tu ya wananchi wa Ufaransa waliotimiza masharti ya kupiga kura na mwakilishi wa asimilia 27 ya wananchi wa nchi hiyo ya bara Ulaya.

Licha ya kuapishwa kwake kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano, Rais Marcon anakabiliwa na changamoto za ndani na nje ya nchi ambazo anatarajiwa kupambana nazo.

Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo ni pamoja na kutekeleza mageuzi aliyoahidi kufanya wakati akichaguliwa kwa awamu ya kwanza mwaka wa 2017 akiwa rais mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa kuongoza Ufaransa.

Changamoto nyingine inayomsubiri rais huyo ni jinsi atakavyoshugulikia uvamizi uliotekelezwa na taifa la Urusi dhidi ya Ukraine.

Suala la kupanda kwa gharama ya maisha nchini mwake pia limetajwa kuwa mojawapo ya changamoto zinamzomsubiri Macron pamoja na jinsi ya kushugulikia suala la umri wafanyakazi wa umma kustaafu.

Laurent Fabius, Mkuu wa baraza la katiba nchini Ufransa amesoma taarifa inayodhinisha ushindi wa Macron katika duru ya pili ya uchaguzi wa tarehe 24 ya mwezi April.

Licha ya sherehe za leo za kuapishwa kwa rais Macron kwa muhula wa pili wa miaka mitano, lakini majukumu yake ofisini yanatarajiwa kuanza rasimi baada ya kumalizika kwa muhula wake wa kwanza ifikapo usiku wa kuamkia tarehe 13 ya mwezi Mei mwaka huu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*