?>

Eslami: Iran imedhamiria kutekeleza miradi yake ya nyuklia

Eslami: Iran imedhamiria kutekeleza miradi yake ya nyuklia

Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran amesisitiza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kmataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuwa Iran imedhamiria kutekeleza miradi yake ya nyuklia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad Eslami leo Jumanne amekuwa na mazungumzo hapa Tehran na waandishi wa habari pamoja na Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa IAEA ambapo amebainisha kuwa suala ambalo limesisitizwa mara kadhaa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ni hili kuwa, hakuna ukengeukaji wowote ulioshuhudiwa katika miradi ya nyuklia ya Iran na kwamba Iran inendesha shughuli zake za nyuklia kwa mujibu wa makubaliano na kanuni zilizowekwa. 

Eslami ameongeza kwamba ni katika ajenda ya kazi kuona kuwa Iran inaweza kustafidi na sekta zote za teknolojia ya nyuklia katika nyanja mbalimbali; na wakala wa IAEA utaisaidia katika suala hilo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki pia ameshukuru mwaliko na mapokezi aliyopata kutoka kwa Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran na kueleza kuwa mazungumzo waliyofanya yalikuwa mazito na kuwa wanaendelea kuyafuatilia ili kuendeleza kazi na mahusiano ili kufikia nyanja za pamoja.  

Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa IAEA jana aliwasili Tehran kwa ajili ya mazungumzo na mashauriano na viongozi wa Iran.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*