Mapigano yanaripotiwa kuendelea katika mkoa wa Tigray, karibu miezi miwili sasa baada ya kuzuka kwa mapigano katika jimbo hilo linalotaka kujitenga.
Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Serikali ya Ethiopia inahakikisha kuwa hali ni shwari katika mkoa huo, lakini ni vigumu kuingia katika jimbo hilo Tigray.
Hata hivyo misafara ya magari ya mashirika ya misaada ya kibinadamu imeendelea kuingiza misaada ya chakula ingawa hali bado ni tete na mawasiliano mpaka sasa yamekatwa.
Vikosi vya Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Tigray ya TPLF pia vinaendelea na vita, kutoka maeneo ya vijijini.
Wakati jeshi la Ethiopia linadhibiti makao makuu ya jimbo la Tigray, hofu inaendelea katika vijiji vya jimbo hilo.
Umoja wa Mataifa unasema mapigano yanaripotiwa mashariki mwa mji wa Mekele, makao makuu ya jimbo la Tigray.
342/