?>

Ethiopia yavionya vyombo vya habari vya Magharibi kwa kueneza porojo

Ethiopia yavionya vyombo vya habari vya Magharibi kwa kueneza porojo

Serikali ya Ethiopia imeyaandikia barua mashirika kadhaa ya habari ya Wamagharibi na kuyaonya vikali dhidi ya kuandika na kueneza habari za kipropaganda zinazoliakisi kwa hasi taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mamlaka ya Vyombo vya Habari Ethiopia imeyaandikia barua mashirika ya habari ya CNN ya Marekani na BBC ya Uingereza, pamoja na Associated Press (AP) na Reuters na kuyakosoa kwa kuandika habari na makala zinazoonekana kwenda sambamba na malengo ya kundi moja la waasi wa nchi hiyo.

Mamlaka hiyo imesema habari za porojo zinazoandikwa na mashirika hayo zinaonekana kuwashabikia na kuwashajiisha wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo.

Mamlaka ya Vyombo vya Habari Ethiopia imesisitiza kuwa, muenendo huo wa vyombo vya habari vya Magharibi unahatarisha maslahi ya serikali ya Ethiopia, mamlaka ya kujitawala na utangamano miongoni mwa wananchi hiyo ya Kiafrika.

Taasisi hiyo ya serikali imesema habari zinazoenezwa na vyombo hivyo vya habari zinakusudia kupanda mbegu za chuki na uhasama miongoni mwa wananchi wa Ethiopia, nchi ambayo inashuhudia mapigano katika maeneo ya kaskazini hususan Tigray.

Mapigano yanayojiri huko Tigray hadi sasa yamesababisha maelfu ya watu kuuawa, huku wengine karibu milioni mbili kuwa wakimbizi, na wengine laki nne kukabiliwa na ukosefu wa chakula. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*