?>

EU yalegeza kamba mbele ya Russia yaachana na mpango wa kuzuia meli zake za mafuta

EU yalegeza kamba mbele ya Russia yaachana na mpango wa kuzuia meli zake za mafuta

Vyombo vya habari vya barani Ulaya vimetangaza kuwa nchi za bara hilo zimelegeza msimamo mbele ya Moscow na sasa hazitoendelea na mpango wake wa kutaka kuzizuia meli za mafuta za Russia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tangu vilipoanza vita huko Ukraine, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU zimeshaiwekea Russia vikwazo vingi vizito. Nchi hizo zimekaribia hata kuiwekea vikwazo vya nishati Russia licha ya kwamba ni tegemezi mno kwa nishati ya nchi hiiyo. Hadi hivi sasa lakini, vikwazo vya nchi za Ulaya dhidi ya Russia vimefeli kutokana na upinzani wa baadhi ya nchi wanachama wa umoja huo.

Jarida la Financial Times limeandika katika ripoti yake kuwa, Umoja wa Ulaya umelazimika kuachana na mpango wake wa kuzuia meli za mafuta za Russia kwani nchi wanachama wa umoja huo zimeshindwa kufikia maafikiano kuhusu jambo hilo.

Jarida hilo pia limeandika, Kamisheni ya Ulaya bado inapenda kuona mashirika ya Ulaya yanaacha kutoa bima kwa meli za mafuta ghafi za Russia ili kwa njia hiyo zipunguze uwezo wa Moscow wa kusafirisha nje mafuta, lakini nchi za Ulaya zimeshindwa kufikia makubaliano kuhusu vikwazo hivyo.

Hivi sasa zaidi ya miezi miwili imepita tangu kuanza vita vya Ukraine hapo tarehe 24 Februari 2022. Nchi za Ulaya nazo zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali dhidi ya Russia ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo vikubwa mpaka kwenye sekta za michezo, lakini linapofika suala la nishati, nchi hizo zinashindwa kufikia makubaliano.

Moscow imeshikilia msimamo wake wa kuziuzia nchi za Ulaya nishati yake kwa sarafu wa Ruble ya Russia na hadi hivi sasa nchi za Ulaya zimeshindwa kuacha utegemezi wao kwa nishati ya nchi hiyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*