?>

Fedheha ya vyombo vya habari na mkanganyiko wa Saudi Arabia katika vita vya Yemen

Fedheha ya vyombo vya habari na mkanganyiko wa Saudi Arabia katika vita vya Yemen

Saudi Arabia, ambayo imeshindwa vita vya Yemen, inaonekana kuchanganyikiwa kutokana na makosa yake katika vyombo vya habari.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mwaka wa saba wa vita vya muungano vamizi wa Saudia dhidi ya Yemen unaelekea kumalizika huku muungano huo ukiendelea kupata vipigo mtawalia kimoja baada ya kingine. Vikosi vya jeshi la Yemen vinazidi kuimarika katika vita vya nchi kavu, anga na majini, na hivi karibuni Wayemen walifanikiwa kusimamisha na kuteka meli inayomilikiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) iliyokuwa na silaha za kivita katika maji ya Yemen. Aidha maeneo ya kaskazini mwa Yemen yamekombolewa kutoka kwenye makucha ya mamluki wa Saudia. Huko kusini mwa Yemen pia kuna serikali mbili, ikiwa ni ile ya kiongozi aliyejiuzulu na kukimbilia Saudia, Mansour Hadi na serikali inayofanya kazi chini ya kivuli cha Baraza la Mpito la Kusini; na licha ya juhudi za Wasaudi, hakuna serikali ya umoja wa kitaifa.

Katika hali hiyo, Wasaudia wamegeukia vita vya vyombo vya habari dhidi ya Wayemen, na vilevile dhidi ya Hizbullah ya Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hapo awali, Wasaudia walionesha mkanda wa video  wakidai kwamba, unamuonesha kamanda wa Hizbullah ya Lebanon akiwa huko Yemen; hata hivyo ilithibitika baadaye kuwa video hiyo ni bandia. Juzi (tarehe 10 Januari) pia Wasaudia walionyesha mkanda mwingine wa video wakidai kuwa video hiyo ni ya ghala la makombora la balistiki la Iran katika bandari ya Al-Hudaydah nchini Yemen. Hata hivyo, filamu hiyo ilikuwa kashfa na fedheha kubwa zaidi kwa Wasaudia kwa sababu mkanda ulioonyeshwa ulikuwa wa filamu ya matukio ya kweli (documentary) ya Marekani kuhusu uvamizi wa Iraq na haina uhusiano wowote na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wala Yemen.

Filamu hizi ni kejeli na fedheha kwa vyombo vya habari vya Saudia kuhusu vita dhidi ya Yemen. Kwa hakika, Wasaudia wanaendesha vita vya vyombo vya habari dhidi ya Hizbullah ya Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakijaribu kutaka kuwashawishi walimwengu waamini kwamba, hawakabiliana na Wayemen pekee  bali pia wanapigana na Iran na Hizbullah, au mtandao wa wanamuqawama. Vita hii ya Wasaudia inafanywa kwa lengo la kupunguza fedheha ya kushindwa kwao huko Yemeni, na katika upande mwingine kwa shabaha ya kufanya propaganda chafu dhidi ya Iran na harakati ya Hizbullah.

Hata hivyo, mbinu hii imetekelezwa na Wasaudia kianagenzi na kuwa kichekesho na fedheha kwao. Mohammad Abdul Salam, mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen, amesema kuhusiana na suala hili kwamba: "Ni kashfa na fedheha kubwa kuona msemaji wa muungano wa wavamizi akikata na kuunganisha vipande vya filamu ya Marekani, na kudai kuwa picha zake ni za eneo la makombora ya Ansarullah huko Al-Hudaydah. Muungano vamizi unataka kufidia hasara zake katika uwanja wa vita kwa kutumia fedheha hii ya vyombo vya habari."

Baada ya mjadala mkali ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mikanda ya video iliyorushwa hewani na Wasaudi, Turki al-Maliki, msemaji wa muungano vamizi huko Yemen amekiri rasmi kwamba mkanda wa video kuhusu ghala la makombora la jeshi la Yemen ni bandia na wa kubuni na kwamba waliupokea kimakosa. 

Mwenendo huu wa Al-Saud unaonyesha kwamba kushindwa kwa Wasaudia katika vita dhidi ya Yemen kumewaacha katika hali ya kuchanganyikiwa na kuwapa kiwewe kiasi kwamba hawawezi kumaizi baina ya sahihi na kisicho sahihi na hatimaye kuwafanya wawe kichekesho kwa walimwengu. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*