?>

Gutteres: Tumuenzi Shujaa Mandela kwa kutafakari kuhusu utu, usawa na haki

Gutteres: Tumuenzi Shujaa Mandela kwa kutafakari kuhusu utu, usawa na haki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewasihi watu wote ulimwenguni kumkumbuka na kumuenzi Shujaa Nelson Mandela kwa kutafakari juu ya utu, usawa, haki, na haki za binadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ujumbe wake katika Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela iliyoadhimishwa jana, Guterres amesema, Nelson Mandela au kwajina lingine Madiba ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini alipenda na kuhimiza mshikamano na kukomesha ubaguzi wa rangi, jambo ambalo sasa lipo hatarini kwani mshikamano wa kijamii ulimwenguni kote unatishiwa na mgawanyiko.

“Kila mwaka, katika siku hii, siku ya kuzaliwa Nelson Mandela, tunamshukuru mtu huyu wa ajabu ambaye alijumuisha matakwa ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa na ulimwengu. Tumeshuhudia sasa jamii zikizidi kuparaganyika, lugha za matusi na uongo zimeongezeka, habari zinazofifisha ukweli, kuhoji sayansi na kudhoofisha taasisi za kidemokrasia.”

Amesema janga linaloendelea la COVID-19 limechangia kurudisha nyuma maendeleo na vita dhidi ya umasikini lakini pia katika kipindi cha matatizo ni wale ambao wapo kwenye makundi yenye kuhitaji msaada ndio wanaoteseka zaidi, na mara nyingi ndio hulaumiwa ilihali hawana hatia kwa yaliyotokea. 

“Janga hilo la Corona limeonesha  umuhimu wa mshikamano na umoja, maadili yaliyopigiwa chapuo na Nelson Mandela katika kipindi chake chote cha uhai akipigania haki.”

“Hakuna aliye salama mpaka wote tuwe salama. Na kila mmoja wetu ana jukumu la kufanya.” Ameongeza Guterres katika ujumbe wake huo. Amehitimisha kwa kusema watu wote wanatakiwa kuhamasika na ujumbe wa Madiba kwamba kila mtu anaweza kuleta mabadiliko katika kutangaza amani, haki za binadamu, maelewano na utu kwa watu wote.

“Katika kuenzi maisha ya Madiba , tuheshimu wito wake na kuchukua hatua na kutiwa nguvu na urithi aliotuachia.”

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*