?>

Haaretz: Jeshi la Israel limekiri kumuuwa Shireen Abu Akleh

Haaretz: Jeshi la Israel limekiri kumuuwa Shireen Abu Akleh

Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni baada ya kufanyika uchunguzi kuhusu kuuliwa ripota wa televisheni ya al Jazeera katika mji wa Jenin limekiri kuwa mwandishi huyo wa habari ameuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni jana waliuvamia mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kumuuwa shahidi Shireen Abu Akleh mwandishi habari Mpalestina huku akiwa amevaa kizibao cha mwandishi habari na kumjeruhi mwenzake Ali al Samud mtayarishaji vipindi.

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, gazeti la Kizayuni la Haaretz leo asubuhi limeripoti kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa Abu Akleh ameuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo baada ya kufanyika uchunguzi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, chunguzi zilizofanywa hadi sasa zimeonyesha kuwa, mwanajeshi mmoja wa kikosi cha siri kwa jina la " Dufdivan" alielekea mahali alipouliwa shahidi Abu Akleh katika umbali wa mita 100 hadi 150 ambapo alifyatua makumi ya risasi kuelekea sehemu hiyo aliyokuwa amesimama shahidi Shireen Abu Akleh.  

Gazeti la Haaretz aidha limeendelea kueleza katika ripoti yake kwamba baadhi ya risasi zilizofyatuliwa na wanajeshi wa Israel wa kikosi chake cha Dufdivan zilipiga katika eneo hilo ambako alikuwepo Shireen  Abu Akleh. Wanajeshi wa utawala wa Kzayuni hadi sasa wamewaua shahidi, kuwatia nguvuni na kuwajeruhi mamia ya waandishi habari wa Kipalestina. 

Kamati ya Kuwaunga Mkono Waandishi Habari wa Palestina hivi karibuni ilitangaza kuwa, utawala wa Kizayuni unatekeleza hatua za kiadui na kiuhasama dhidi ya waandishi wa habari lengo likiwa ni kuzuia kufichuliwa jinai za utawala huo haramu dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*